general1836 wordsRead on Arc Codex

Wairan waanza kumuaga Khamenei mashaka yakiongezeka kuhusu hatima ya Mojtaba

Ali Azmaei ateuliwa kamanda wa Jeshi la majini la IRGC Ali Azmaei ametambulishwa kama kamanda mpya wa Jeshi la Wanamaji la IRGC. Kamanda wa awali wa jeshi hilo alikuwa Alireza Tangsiri, ambaye aliuawa tarehe 26 Aprili katika shambulio la Marekani na Israel dhidi ya Iran. Hapo awali, Ali Azmaei alikuwa kamanda wa kitengo chaTano cha Jeshi la Wanamaji la IRGC. Kitengo hicho kilianzishwa tarehe 4 Novemba 2012, na lilikuwa likiendesha shughuli zake "kuanzia ncha ya Kisiwa cha Qeshm, pamoja na eneo la Visiwa vya Nazeat, hadi magharibi mwa Kisiwa cha Kish." Bw. Azmaei aliteuliwa kuwa kamanda wa kitengo hicho tangu kilipobuniwa Kabla ya hapo, alikuwa naibu kamanda Kikosi cha Kwanza cha Jeshi la Wanamaji la IRGC. Taylor Swift na Travis Kelce wafunga ndoa jijini New York Baada ya miezi kadhaa Taylor Swift na Travis Kelce hatimaye wamefunga ndoa katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini New York, Marekani Taarifa hizo Habari hizo zilithibitishwa Ijumaa jioni na msemaji wa Swift,huku skrini kubwa nje ya ukumbi huo zikionyesha ujumbe: "JUST&T MARRIED!" Swift, ambaye ni nyota mkubwa zaidi wa muziki wa pop duniani, na Kelce, bingwa mara tatu wa Super Bowl, walivishana pete ya uchumba Agosti mwaka iliyopita, na tangu wakati huo mashabiki wamekuwa wakijiuliza ndoa itafungwa lini, wapi na vipi tukio hilo lingefanyika. Hafla hiyo ya siku mbili ilisababisha mojawapo ya maeneo yenye shughuli nyingi zaidi jijini New York kufungwa, huku orodha ya wageni ikijumuisha msururu wa mastaa wakubwa kama vile Selena Gomez, Camila Cabello, Hugh Grant, Gracie Abrams, Ellie Goulding, Graham Norton na Dakota Johnson. Hakuna picha rasmi zilizotolewa kutoka ndani ya ukumbi huo, na wengi kati ya waliohudhuria—wanaokadiriwa kufikia 1,000—waliingia bila kupigwa picha, ingawa baadhi yao walionekana wakati wakiingia na kutoka. Mazishi ya Ali Khamenei: Mojtaba Khamenei hataongoza sala ya mazishi Vyombo vya habari vya Iran vinasema kuwa "marja'i taqlid" (kiongozi wa kidini mwenye mamlaka ya kutoa mwongozo wa kisheria) ataongoza sala za mazishi ya Ali Khamenei na familia yake. Jafar Sobhani Tabrizi ataongoza sala za mazishi mjini Tehran, Nasser Makarem Shirazi mjini Qom, na Hossein Nouri Hamedani mjini Mashhad. Ali Akbar Pourjamshidian, katibu wa kamati ya maandalizi ya mazishi ya Ali Khamenei, alikuwa amesema kuwa uamuzi kuhusu kuhudhuria kwa Mojtaba Khamenei katika mazishi ya baba yake ulikuwa mikononi mwa familia ya Kiongozi Mkuu, na iwapo ingepangwa hivyo, taarifa ingetolewa kupitia ofisi yake. Mojtaba Khamenei hajaonekana hadharani tangu kuanza kwa vita, wakati baba yake na jamaa zao kadhaa walipouawa mwanzoni mwa vita hivyo vya siku 40, na hakuna rekodi yoyote ya sauti au video yake iliyotolewa. Wairan wamuaga Khamenei mashaka yakiongezeka kuhusu hatima ya Mojtaba Mazishi ya hadhara ya Kiongozi Mkuu wa zamani Ali Khamenei yalianza nchini Iran Jumamosi, zaidi ya miezi minne baada ya kifo chake katika siku ya kwanza ya vita vya Marekani na Israel. Maelfu walikusanyika kwenye ukumbi wa maombi wa Imam Khomeini kuaga mwili wa Khamenei, kuanzia saa 6:00 asubuhi Jumamosi, huku miito ya kulipiza kisasi kwa mauaji yake ikitanda hewani. Maafisa wa Iran pia walitoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kama ishara ya "kulilaani kuuawa kwa kiongozi mkuu wa nchi." Khamenei anazikwa pamoja na jamaa zake wanne waliouawa pamoja naye, akiwemo mke wa mwanawe Mojtaba, chini ya ulinzi mkali. Usalama umedumishwa katika mji mkuu na miji ningige mikubwa ya Iran. Rais wa Marekani Donald Trump alidokeza kwamba ameipa Iran muda wa wiki moja wa kufanya mazishi ya Kiongozi Mkuu. ''"Tuliipatia Iran pigo kubwa sana," Trump alisema katika hotuba yake siku ya Jumamosi wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 250 tangu kuanzishwa kwa Marekani. "Wana hamu kubwa ya kufikia makubaliano; wanataka sana kufanya hivyo. Tuliwapa muda wa wiki moja kumzika kiongozi wao." Kuhusu vita alivyovianzisha na kuvimaliza, rais huyo wa Marekani alieleza kuwa aliijumuisha Iran katika orodha hiyo licha ya kuwa na mashaka makubwa kuhusu mustakabali wa makubaliano yoyote ya amani. Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, aliandika kwenye mtandao wa X: "Wakati Iran—nchi yenye historia tukufu na ya kishujaa—ikijiandaa kumuaga Kiongozi wake, natoa wito kwa wananchi wote, bila kujali kabila, dini, au msimamo wa kisiasa, kuonyesha taswira thabiti ya umoja wa kitaifa na utiifu kwa misingi mikuu ya mfumo wa Kiislamu, kupitia tukio hili la kihistoria." Zaidi ya wakimbizi 600,000 wa Lebanon wamerejea makwao- IOM Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa zaidi ya wakimbizi 600,000 wa Lebanon wamerejea majumbani mwao baada ya mapigano yakipungua kufuatia makubaliano ya kusitisha vita katika eneo la Mashariki ya Kati. Katika ripoti yake, shirika hilo lilisema kuwa takriban watu 500,000 bado ni wakimbizi wa ndani na hawajaweza kurejea makwao. Takwimu hizo zinatokana na taarifa zilizokusanywa tangu tarehe 22 Juni kwa kushirikiana na mamlaka za eneo hilo. Lebanon ilijikuta katika vita vya kikanda mapema mwezi Machi (miezi minne iliyopita), wakati kundi la Hezbollah—linaloungwa mkono na Tehran—liliporusha makombora dhidi ya Israel kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi mkuu wa Iran Ayatolla Ali Khamenei katika mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel. Jeshi la Tanzania latoa onyo dhidi ya wavunjifu wa amani Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa litachukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu watakaojihusisha na vitendo vinavyohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani. Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192. Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na matukio yoyote ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani. Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu viashiria vya uchochezi ili kudumisha utulivu nchini. Jeshi pia limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda mipaka, Katiba na mamlaka ya nchi sambamba na kushirikiana na wananchi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya taifa. Colombia iliifunga Ghana bao 1-0 na kufuzu kwa hatua ya 16 ya Kombe la Dunia kupitia bao lililofungwa na John Arias katika raundi ya timu 32 Arias alifunga bao hilo katika dakika ya 14 kwa shuti la karibu kufuatia pasi kutoka kwa Luis Suarez, ambaye ndio mwanzo alikuwa ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya John Cordoba aliyeumia. Luis Diaz alidhani ameongeza bao la pili dhidi ya Colombia katika dakika ya 56, lakini mwamuzi alilikataa bao hilo kwani alikuwa ameotea. Colombia ilitawala sehemu kubwa ya mchezo, huku kipa wa Ghana akifanya kazi nzuri ya kuokoa mikwaju mitatu hatari. 'Sharks' wa Cape Verde wawatikisa mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Cape Verde ilimaliza mbio yake ya kuwania Kombe la Dunia kwa kumaliza kishujaa, nusura kuwaondoa mabingwa watetezi, lakini Argentina, ikiongozwa na gwiji wao Lionel Messi, ilipata ushindi mgumu wa 3-2 baada ya muda wa ziada. Timu hiyo ya taifa ya visiwa vya Atlantiki, yenye idadi ya watu nusu milioni pekee, imekuwa kivutio kikubwa baada ya kukaidi matarajio kwa kutoka sare na mabingwa wa Ulaya Uhispania kabla ya kupata nafasi ya kuingia raundi inayofuata, ikimaliza mbele ya mabingwa mara mbili wa dunia Uruguay na Saudi Arabia katika Kundi H. Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, alisema kuwa kupoteza mechi dhidi ya Cape Verde "ingelikuwa jambo la ajabu sana". Scaloni aliongeza: "Ulikuwa mchezo mgumu sana; kilichotuwezesha kupata ushindi ni hulka ya timu hii (Argentina) haikati tamaa kamwe." Aliendelea kusema: "Tunawapongeza wapinzani wetu, kwa sababu wakati watu wakisema hakuna wapinzani dhaifu, leo wao wamethibitisha kuwa ni timu imara." Argentina inatarajia kuwa timu ya kwanza tangu mwaka 1962 kutetea taji lake la dunia. Baada ya Messi kufungua ukurasa wa mabao—akifunga bao lake la saba katika mashindano haya na kuongoza orodha ya wafungaji huku akifikisha jumla ya mabao 20 katika historia yake ya Kombe la Dunia—Deroy Duarte alijibu kwa kusawazisha matokeo. Kombe la Dunia 2026: Misri kukutana na Argentina katika hatua ya 16 Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Misri imefuzu kwa hatua ya 16 michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuishinda Australia kwa penalti 4-2 (baada ya sare ya 1-1) siku ya Ijumaa mjini Dallas, Marekani. Misri sasa itakutana na mabingwa watetezi Argentina, ambao walinusurika kwa shida dhidi ya Cape Verde, kwa ushindi wa 3-2 katika muda wa nyongeza. Wachezaji wa timu ya 'Mafarao' walilipuka kwa furaha baada ya Hossam Abdel-Maguid kufunga penalti ya nne, huku sherehe zikianza kushuhudiwa miongoni mwa wachezaji na mashabiki viwanjani Arlington mbele ya watazamaji 80,000, wakati timu hiyo ikifikia mafanikio mapya. Kombe hili la Dunia ndilo lenye mafanikio makubwa zaidi kwa Misri katika mashindano manne (1934, 1990 na 2018), baada ya kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya New Zealand (3-1) katika hatua ya makundi na kufuzu kwa raundi ya mtoano kwa mara ya kwanza. Misri imekuwa nchi ya tano barani Afrika kufuzu kutoka hatua ya mtoano, baada ya Cameroon (1990), Senegal (2002), Ghana (2010) na Morocco (2022 na 2026). Panenka ya nyota Mohamed Salah iliiwezesha Misri kuongoza kwa mabao 3-2. Marekani yawaondoa wanajeshi wake Nigeria baada ya operesheni dhidi ya Islamic State Marekani imewaondoa wanajeshi wake waliopelekwa nchini Nigeria mapema mwaka huu katika juhudi za kusaidia kupambana na makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali za kidini. Mnamo Desembam waka jana, vikosi vya Marekani na Nigeria vilianzisha operesheni ya pamoja katika eneo la Bonde la Ziwa Chad, ambayo ilihusisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo siku ya Krismasi, na kufuatiwa na kutumwa kwa wanajeshi 200 miezi miwili baadaye. Kiongozi mkuu wa Islamic State (IS) Abu-Bilal al-Minuki aliuawa wakati wa operesheni hiyo iliyodumu kwa miezi kadhaa. Siku ya Alhamisi, Marekani iliangazia mafanikio yaliyofikiwa katika operesheni hiyo, huku msemaji wa jeshi la Nigeria akiiambia BBC kuwa kujiondoa kwa wanajeshi wa Marekani "hakutaathiri kasi yetu kwa vyovyote vile". Licha ya oparesheni hizo, makundi ya kijihadi yameendelea na mashambulizi hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria. Meja Jenerali Michael Onoja alisema ushirikiano wa kijasusi kati ya nchi hizo mbili utaendelea, jambo ambalo jeshi la Marekani pia lilisema katika mkutano wake. Ushirikiano wa kijeshi kati ya Nigeria na Marekani uliongezeka baada ya Washington kushutumu mamlaka ya Nigeria kwa kushindwa kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kijihadi, na kudai kulikuwa na "mauaji ya kimbari dhidi ya waumini wa Kikristo" nchini humo. Nigeria imekanusha madai hayo, ikisema ghasia hizo zinaathiri watu kutoka jamii zote. Mazishi ya Ali Khamenei yaanza rasmi kwa kufunguliwa kwa msikiti wa Tehran Vyombo vya habari vya Iran vinasema kuwa kadiri idadi ya watu inavyoongezeka katika eneo la Mosalla mjini Tehran, milango ya kaskazini ya eneo hilo imefunguliwa pia kwa ajili ya washiriki wa mazishi ya Ali Khamenei, kiongozi Mkuu wa zamani wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu aliyeuawakatika mashambulizi ya Marekani na Israel. Jeneza la Khamenei linatarajiwa kuwekwa hadharani katika msikiti wa Mosalla mjini Tehran, ambapo watu watapita fursa ya kuliona. Maafisa wa Iran wanasema wanatarajia watu kati ya milioni 15 na 20 kuhudhuria shughuli hiyo ya siku sita katika miji mbalimbali nchini Iran na Iraq. Wakati huo huo, vyanzo vya habari nchini Iraq vinasema kuwa Baghdad, mji mkuu wa nchi hiyo, utasitisha shughuli zake kwa siku ya Jumatano kwa ajili ya mazishi ya Ali Khamenei. Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, shughuli hiyo itahitimishwa kwa mazishi ya Bw. Khamenei katika mji wake wa asili wa Mashhad siku ya Alhamisi. Ayatollah Ali Khamenei aliuawa pamoja na jamaa wanne wa familia yake mwanzoni mwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

How it works

Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.

Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.