Je, Israel iko karibu kuanzisha kambi ya kijeshi huko Somaliland?
Je, Israel iko karibu kuanzisha kambi ya kijeshi huko Somaliland?
Matamshi ya Rais wa Somaliland Abdulrahman Mohamed Abdullahi Araujo katika ziara yake mwezi Juni nchini Israel kuhusiana na uwezekano wa kuanzisha kituo cha kijeshi cha Israel katika eneo hilo yamezua mjadala mkubwa.
Matamshi ya rais wa Somaliland kwa mara nyingine tena yamevuta hisia kwenye vituo viwili vya kimkakati eneo la Berbera, kwenye uwanja wa ndege wa Berbera na bandari yake mpya iliyo karibu, ambayo imeshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo katika miaka ya hivi karibuni.
Somaliland, ambayo ilitangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991 ipo uhuru licha ya kukosa kutambulika kimataifa, ipo kwenye lango la Bahari ya shamu na mojawapo ya njia muhimu zaidi za bahari.
Timu ya kudhibitisha habari ya BBC ilichunguza picha za satelaiti za uwanja wa ndege wa Berbera na kituo cha majini kilicho karibu.
Picha hizo zinaonyesha kuwa shughuli za ujenzi na uchimbaji visima zimekuwa zikiendelea katika eneo hilo kwa miaka mingi, na hivyo kuzua maswali kuhusu iwapo shughuli hizi ni sehemu ya maendeleo ya miundombinu na miradi ya kibiashara, au kama zinaweza kutengeneza njia kwa matumizi ya kijeshi ya siku zijazo.
Katika kukabiliana na utambuzi wa Israel wa Somaliland, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ilitangaza kwamba hatua hii ililenga "kuwezesha mipango ya kulazimishwa ya kuwahamisha Wapalestina."
Ziara ya Israel
Ziara ya Abdulrahman Mohamed Abdullahi Arru nchini Israel ilizua maswali kuhusu kiwango cha usalama na ushirikiano wa kijeshi unaotarajiwa kati ya pande hizo mbili, hasa baada ya kusema katika mahojiano ya televisheni kwamba kujengwa kwa kambi ya kijeshi ya Israel Somaliland "hakujafutiliwa mbali"
Maoni hayo yanajiri miezi kadhaa baada ya Israel kuitambua Somaliland, eneo ambalo lilijitangazia uhuru wake kutoka kwa serikali kuu ya Mogadishu mwaka 1991.
Wakati wa ziara yake,Waziri wa Ulinzi wa Somaliland, Mohamed Yusuf, pia alitangaza kuwa Israel inatoa mafunzo kwa vikosi vya polisi na jeshi vya eneo hilo.
Picha za setilaiti za Berbera zinaonyesha nini?
Timu ya kudhibitisha habari ya BBC ilichunguza picha za setilaiti za uwanja wa ndege wa Berbera, ambazo zinaonyesha shughuli kubwa za ujenzi katika uwanja wa ndege katika miaka michache iliyopita. Bandari mpya pia imejengwa karibu na uwanja wa ndege.
Picha hizo zinaonyesha upanuzi mkubwa katika uwanja wa ndege. Mnamo 2018, uwanja wa ndege ulikuwa na njia ya awali ya ndege, lakini picha za Mei mwaka huu zinaonyesha njia ya safari za ndege sasa imekamilika.
Kulingana na wataalamu waliozungumza na BBC, urefu wa njia hii ya ndege ni kwamba itaruhusu matumizi ya ndege za kiraia na za kijeshi.
Zaidi ya hayo, ujenzi mpya unaonekana karibu na sehemu ya vifaa vya uwanja wa ndege, ambayo inaweza kuwa ya maeneo ya rubani.
Israel inataka nini Somaliland?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kulingana na wachambuzi, Israel inaichukulia Pembe ya Afrika kama sehemu ya moja kwa moja ya usalama wa Bahari ya Shamu na imekuwa ikijitahidi kwa miongo kadhaa kujenga mtandao wa mahusiano ya kisiasa na kiusalama na nchi za eneo hilo.
Lengo la sera hii ni kulinda njia za usafirishaji wa meli na kuimarisha ushawishi wa Israel katika eneo hilo.
Uwanja wa Ndege wa Berbera una eneo la kimkakati kwa ajili ya kufuatilia mwendo wa meli katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamu, na upo karibu na Mlango-bahari wa Bab al-Mandab.
Eneo hilo pia liko karibu na maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen; Berbera iko umbali wa takriban kilomita 550 pekee kutoka Sanaa.
Orna Mizrahi, mtafiti katika Taasisi ya Israel ya Mafunzo ya Usalama wa Taifa, aliambia BBC: "Umuhimu wa Somaliland kwa Israel umeongezeka kutokana na mgogoro na Wahouthi. Wahouthi walianza kurusha makombora kuelekea Israel, na jambo hili liliifanya Israel ielewe umuhimu wa kupanua mahusiano na Somaliland ili kufuatilia vyema hali ya mambo nchini Yemen."
"Hilo ndilo lilikuwa kichocheo kikuu," aliongeza. "Tulijaribu kuimarisha mahusiano yetu na Somaliland kwa sababu inaiwezesha Israel kuwa na faida ya kimkakati kuhusiana na bara zima la Afrika. Yemen iko ng'ambo ya maji, na hali hiyo inaruhusu Israel kuwa na uwepo katika eneo hilo, kufuatilia matukio upande wa pili, kufanya shughuli za kijasusi na ufuatiliaji, na kuelewa vyema mienendo ya Wahouthi. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi."
How it works
Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.
Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.