general3360 wordsRead on Arc Codex

Raia wa kigeni nchini Kenya wana siku 90 kuwa na vibali vya kazi

Raia wa kigeni nchini Kenya wana siku 90 kuwa na vibali vya kazi Kenya imewapa raia wa kigeni wanaoendesha biashara ndogo ndogo siku 90 za kuratibu hadhi yao ya uhamiaji, vibali vya kazi na leseni za biashara. Muhtasari - Iran yasema imekamata nyambizi ya Marekani - Israel imechukua hatua gani kufuatia uamuzi wa vikwazo vya Uingereza? - Alichokisema Andy Burnham kuhusu uhusiano wa Uingereza na Israel - Waziri wa Mawasiliano Iran: Vituo 500 vya mawasiliano viliharibiwa vitani - 'Vikwazo si suluhisho,' asema Rais wa Israel. - Raia wa kigeni nchini Kenya wana siku 90 kuwa na vibali vya kazi - Wanamgambo wa Houthi wa Yemen: Tumeshambulia maeneo ya kiuchumi na kijeshi ya Saudi Arabia - "Wanafunzi na wazazi wana hofu," asema mwalimu wa shule katika Ukingo wa Magharibi - Canada yaanza kutoza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa za Marekani - Urusi na Korea Kaskazini zafungua daraja la kwanza la barabara kuunganisha nchi hizo - Kenya yatoa msamaha wa muda kwa raia wa Afrika Mashariki wasio na nyaraka - Kenya yaomba radhi kwa Warundi, yaahidi kuwalinda - Mbappé ajitosa katika kinyang'anyiro cha Ballon d'Or - IRGC yatishia meli zinazotumia njia ya kusini ya Hormuz - Tetesi za Soka Jumanne: Chiesa kuondoka Liverpool - Iran yasema ina uwezo wa kuzishambulia meli za kivita za Marekani Moja kwa moja Na Mariam Mjahid & Sarafina Robi Iran yasema imekamata nyambizi ya Marekani Shirika la habari la Fars, ambalo lina uhusiano wa karibu na jeshi, linasema limekamata nyambizi ya kisasa ya Marekani inayojiendesha yenyewe. Kwa mujibu wa Fars, hii ni mojawapo ya nyambizi za kisasa zaidi, zenye teknolojia ya akili mnemba yani AI na zisizo na rubani zinazotumiwa na jeshi la Marekani. Fars inasema kuwa ilinasa chombo hicho katika eneo la "ingilio la mlango bahari wa Hormuz." Marekani bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hii. Pia unaweza kusoma: Israel imechukua hatua gani kufuatia uamuzi wa vikwazo vya Uingereza? Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, ametoa msimamo wa Israel kuhusiana na tangazo la Uingereza la kuweka vikwazo. Haya ndiyo aliyoyasema: Saar aliielezea serikali ya sasa ya Uingereza kama serikali "yenye uadui" ambayo "inachukua hatua za kimfumo" dhidi ya Israel. Akirejelea tangazo la leo hasa, aliishutumu Uingereza kwa "kuingilia kati waziwazi" mchakato wa uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini Israel mwezi ujao. Waziri huyo wa mambo ya nje pia aliishutumu serikali hiyo kwa kuchangia kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi. Kuhusu ujenzi wa makazi ya E1, jambo ambalo Miliband alisema awali Uingereza inataka kulizuia, Saar alisema leo kuwa hakuna maamuzi mapya yaliyofikiwa kuhusu suala hilo akirudia kuishutumu serikali kwa kujaribu kushawishi mambo wakati wa kampeni za uchaguzi. Hatua nne za kulipiza kisasi zilizotangazwa na Saar ni pamoja na kufungwa kwa Ubalozi Mdogo wa Uingereza mjini Jerusalem na kuondolewa kwa wawakilishi wa Uingereza kutoka Kituo cha Kimataifa cha Kusaidia Gaza. Kiongozi anayelipwa mshahara wa juu zaidi duniani kupata nyongeza ya dola milioni 1 Serikali ya Singapore imesema itaongeza mishahara ya kila mwaka ya mawaziri wake na viongozi wengine wa umma, akiwemo Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi wa kisiasa anayelipwa mshahara wa juu zaidi duniani. Lawrence Wong atapata ongezeko la dola za Singapore milioni 1.4 (dola za Marekani milioni 1.1; pauni 818,000) katika jumla ya mapato yake ya kila mwaka. Amesema atatoa ongezeko hilo la mshahara kwa ajili ya misaada ya kijamii katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Wong alisema kuwa kuongeza mishahara ya mawaziri ni muhimu ili kuvutia watu wenye uwezo mkubwa na ujuzi wa hali ya juu. Hapo awali, serikali imekuwa ikisema kuwa kuwalipa mawaziri mishahara mikubwa husaidia kuzuia rushwa. Hata hivyo, hatua hiyo imezua ukosoaji nchini Singapore, ambako kuna wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa ajira na kupanda kwa gharama za maisha. Hata kabla ya ongezeko hilo la mshahara kuanza kutekelezwa, Wong tayari ndiye kiongozi wa dunia anayelipwa mshahara wa juu zaidi kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa anapokea mshahara wa kila mwaka wa dola za Singapore milioni 2.2, na sasa mshahara wake utapanda kwa zaidi ya asilimia 60 na kufikia dola za Singapore milioni 3.6 (dola za Marekani milioni 2.8). Anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Hong Kong, John Lee, anayepata takriban dola 719,000, akifuatiwa na Rais wa Uswizi, Guy Parmelin, anayepata dola 606,000. Rais wa Marekani Donald Trump hupata dola 400,000 kwa mwaka, huku Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham akipata dola 230,000. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 12 watoa taarifa ya pamoja kuhusu vikwazo vya kibiashara Habari za hivi punde Mapema, Miliband alisema kuwa Ufaransa na Kanada nazo zingetangaza marufuku ya uingizaji wa bidhaa kutoka katika makazi haramu. Taarifa ya pamoja kutoka kwa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 12 imetolewa hivi punde, ikielezea nia yao ya kuweka vikwazo vya kibiashara dhidi ya makazi hayo haramu. Nchi hizo ni: Ufaransa, Uingereza, Kanada, Denmark, Uhispania, Ufini, Ireland, Iceland, Norway, Poland, Ureno na Uswidi. Taarifa hiyo inasisitiza kuwa suluhisho la mataifa mawili lazima lilindwe na kuitaka serikali ya Israel kusitisha mara moja upanuzi wa makazi hayo. Qatar yajaribu "kurejesha mazungumzo" kati ya Iran na Marekani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ametangaza kuwa nchi hiyo inashirikiana "na washirika wake katika eneo hili na kote duniani, akiwemo China," ili kurejesha mazungumzo kati ya Marekani na Iran. Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar kwa sasa anaongoza ujumbe uliosafiri kwenda Beijing. Pakistan kwa sasa ndiyo mpatanishi mkuu kati ya Iran na Marekani, lakini maafisa wa Qatar pia wanashiriki kikamilifu katika upatanishi huo, kulingana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hapo awali tuliripoti kuwa ujumbe wa kidiplomasia wa Qatar ulisafiri hivi karibuni kwenda Iran. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema jana kuwa ujumbe huo ulikutana na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araqchi na kueleza kuwa lengo la ziara hiyo lilikuwa "kuendeleza juhudi za kupunguza mvutano" katika eneo hilo. Uingereza yaanzisha vikwazo vipya na vikali zaidi dhidi ya Iran Leo (Jumanne, Septemba 8),Uingereza imetangaza sheria ya kuweka vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran, ikipanua wigo wa vikwazo vya kibiashara na mamlaka ya kulenga meli. Hatua hizi zimeelezwa kuwa sehemu ya juhudi pana zaidi za kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran na shughuli nyingine za uhasama. Serikali ya Uingereza inasema hatua hizo zitazuia Iran kufikia mfumo wa kifedha wa Uingereza na kupanua marufuku ya kibiashara ili kujumuisha bidhaa, teknolojia na huduma zaidi. Hatua hizo pia zitapiga marufuku ndege za Iran kutua katika ardhi ya Uingereza, isipokuwa katika hali maalum. Stephen Doughty, afisa mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, alisema katika taarifa kwamba sheria hiyo "inaimarisha juhudi zetu za kudhibiti malengo ya Iran ya kumiliki silaha za nyuklia" na itasaidia London kuhakikisha kuwa Iran haiwezi kamwe kupata silaha ya nyuklia. Uingereza kupiga marufuku bidhaa kutoka maeneo yanayokaliwa na Israel katika ukingo wa Magharibi Serikali ya Uingereza inapanga kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa zinazozalishwa katika makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi na Bonde la Jordan, ikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo. Hatua hii ni sehemu ya mfululizo wa mabadiliko ambayo serikali ya Uingereza inapanga kufanya katika sera yake kuelekea Israeli, kwani inaongeza shinikizo juu ya suala la kupanua makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi na Bonde la Jordan. Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Ed Miliband aliwaambia wabunge kwamba serikali inapanga kubadilisha baadhi ya sera zake na Israeli. Serikali za awali za Uingereza zimeelezea makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kama yanayokiuka sheria za kimataifa, zikisema kwamba upanuzi wao unaweza kudhoofisha amani na uanzishwaji wa majimbo mawili. Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Israeli alionya kwamba Uingereza ilikuwa ikijiandaa kufanya kosa, akisema itakabiliwa na jibu kutokana na hatua hiyo. Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham pia alizungumza na Rais wa Marekani Donald Trump na washirika wengine muhimu, ikiwa ni pamoja na Qatar, Jumatatu ili kuwafahamisha kuhusu mipango ya serikali ya Uingereza kwa eneo hilo. Uingereza yakubali kuna mauaji ya kikabila katika Ukingo wa Magharibi Akiendelea kuzungumzia makazi katika Ukingo wa Magharibi, Miliband anarejelea ufafanuzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kikabila. Anasema serikali ya Uingereza "inakubali" kuwa kuna mauaji ya kikabila katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi. Anawaambia wabunge kuwa, mara nyingi serikali ya Israel imejifanya kutoliona suala hili. Anaendelea kusema kuwa, kwa muda mrefu serikali ya Uingereza imekuwa ikisema makazi hayo ni kinyume cha sheria. "Leo ninatangaza msimamo rasmi wa serikali ya Uingereza kwamba uvamizi huo ni kinyume cha sheria." Alichokisema Andy Burnham kuhusu uhusiano wa Uingereza na Israel Muda mfupi kabla ya kuwa Waziri Mkuu mnamo mwezi Julai, Andy Burnham aliomba radhi kwa jinsi chama cha Labour kilivyoshughulikia awali hatua za kijeshi za Israel huko Gaza, akisema chama hicho "hakikufanya uamuzi sahihi". Pia alisema kuwa kuna haja ya kufanya zaidi ili "kuhakikisha serikali ya Israel inazingatia sheria za kimataifa na kudumisha matumaini ya suluhisho la mataifa mawili". Hapo awali, chama cha Labour kilipoteza uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wafuasi wake wa mrengo wa kushoto kutokana na msimamo wa awali wa Keir Starmer kuhusu vita vya Gaza. Katika wiki za awali za mzozo huo, Starmer aliunga mkono kusitishwa kwa mapigano kwa muda ili kuruhusu misaada kuwafikia wakazi wa Gaza, lakini hakufikia hatua ya kutaka kusitishwa kabisa kwa mapigano. Tangu wakati huo, Burnham amesema kuwa "Uingereza ilichelewa mno kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano". Pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu mpango wa ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la E1, akisema bungeni wiki iliyopita kuwa hatua hiyo inaweza "kuhatarisha" au "kuhitimisha" suluhisho la mataifa mawili. Pia unaweza kusoma: Waziri wa Mawasiliano Iran: Vituo 500 vya mawasiliano viliharibiwa vitani Sattar Hashemi, Waziri wa Mawasiliano wa Iran, alitangaza katika kikao cha hadhara cha bunge siku ya Jumanne, tarehe 8 Septemba, kwamba kutokana na kusitishwa kwa huduma za intaneti katika miezi ya hivi karibuni, mapato ya sekta ya mawasiliano yamepungua kwa kiasi kikubwa. Hashemi alisema kuwa kufuatia kusitishwa kwa intaneti, Wizara ya Mawasiliano imeshuhudia kushuka kwa mapato kwa asilimia 30 katika sekta ya mawasiliano ya kudumu, na asilimia 50 katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi. Alibainisha kuwa asilimia 70 ya vifaa vya mawasiliano nchini vinategemea fedha za kigeni, na akataja suala la upatikanaji wa fedha za kigeni pamoja na usambazaji wa vifaa katika hali ya sasa ya nchi kuwa changamoto na tatizo kubwa kwa Wizara ya Mawasiliano. Hashemi pia alisema kuwa wakati wa vita vilivyodumu kwa siku 40, vituo 500 vya mawasiliano nchini vilishambuliwa na kuharibiwa. Pia unaweza kusoma: 'Vikwazo si suluhisho,' asema Rais wa Israel. Mpango wa serikali ya Uingereza wa kuweka vikwazo vya kibiashara dhidi ya makazi ya Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi unaodhibitiwa kimabavu ni "makosa makubwa ya tathmini," anasema Rais wa Israel. Akizungumza kutoka Jerusalem siku ya Jumanne, Isaac Herzog anasema uamuzi huo utaonekana kuwa "wa upande usio sahihi wa historia," na kuongeza, "Katika muktadha wa sasa, itakuwa ni uingiliaji mkubwa katika uchaguzi wa kidemokrasia wa taifa huru." Herzog anasema hatua hiyo itawaathiri moja kwa moja Wapalestina na kuzihimiza serikali za kigeni kuelekea kwenye "mazungumzo yenye tija" na ushirikiano. "Vikwazo si suluhisho," anasema. Raia wa kigeni nchini Kenya wana siku 90 kuwa na vibali vya kazi Kenya imewapa raia wa kigeni wanaoendesha biashara ndogo ndogo siku 90 za kuratibu hadhi yao ya uhamiaji, vibali vya kazi na leseni za biashara. Katika taarifa, Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed alisema zoezi hilo litaratibiwa na balozi za raia walioathiriwa, na kuwapa "fursa iliyo wazi na iliyopangwa ya kuratibu" hadhi yao na shughuli za biashara. "Katika siku 90 zijazo, Serikali itafanya zoezi la kuratibu kwa utaratibu ili kurahisisha uzingatiaji," ilisoma taarifa hiyo. Baada ya kipindi cha siku 90, mahitaji ya uhamiaji, kibali cha kazi, usajili na leseni "yatatekelezwa kwa uthabiti na kwa ukali kulingana na sheria na mchakato unaostahili". Tangazo hilo linafuatia agizo la awali la Rais William Ruto kwamba biashara ndogo ndogo kama vile uuzaji wa bidhaa nje na rejareja zinapaswa kutengwa kwa ajili ya Wakenya, na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyabiashara wa kigeni, haswa Warundi. Serikali pia inatafuta kupanua Muswada wa Maudhui ya Ndani, ambao kwa sasa uko Bungeni, ili kuunda kile inachokiita "mfumo ulio wazi, wa haki na unaotabirika" wa kushiriki katika biashara ndogo ndogo. Mabadiliko yaliyopendekezwa yatatambua shughuli za kiuchumi ambazo zinaweza kutengwa kwa ajili ya raia wa Kenya, huku yakiwalinda raia wa kigeni walio na haki halali ya kufanya kazi, kuwekeza au kufanya biashara nchini Kenya. Serikali pia imeonya dhidi ya unyanyasaji au vitisho dhidi ya raia wa kigeni. "Wasiwasi kuhusu fursa za kiuchumi hauwezi kamwe kuhalalisha ubaguzi, kuhalalisha uvunjaji wa sheria au kuidhinisha vurugu." Inafuatia siku ya iliyojaa sintofahamu jijini Nairobi, ambapo mamia ya Warundi walikusanyika katika ubalozi wao huku kukiwa na hofu kuhusu agizo hilo. Serikali ya Burundi pia iliibua wasiwasi kuhusu jinsi raia wake wanavyotendewa. Pia unaweza kusoma: Wanamgambo wa Houthi wa Yemen: Tumeshambulia maeneo ya kiuchumi na kijeshi ya Saudi Arabia Wanamgambo wa Houthi wa Yemen walitangaza kuwa wamerusha makumi ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya maeneo ya kiuchumi na kijeshi nchini Saudi Arabia, ikiwa ni jibu kwa kile walichokiita mashambulizi zaidi ya 120 ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen katika kipindi cha siku tatu zilizopita. "Vikosi vya jeshi la Yemen vilifanya operesheni kubwa ya kijeshi ya masafa marefu kwa kutumia makumi ya makombora ya balistiki na ndege zisizo na rubani," alisema Yahya Saree, msemaji wa kijeshi wa Houthi. Awali tuliripoti kuwa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen ulitangaza kuwa angalau watu 73 walijeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya Saudi Arabia. Muungano huo ulitangaza kuwa utachukua hatua madhubuti kujibu mashambulizi hayo. Wanamgambo wa Houthi, ambao wanadhibiti maeneo yenye watu wengi zaidi nchini Yemen na sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi hiyo, wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia na kulenga meli zake katika Bahari ya Shamu tangu walipotangaza kuzuia usafiri wa majini kwenda nchi hiyo mwezi Julai. "Wanafunzi na wazazi wana hofu," asema mwalimu wa shule katika Ukingo wa Magharibi Watu sita, wakiwemo wanafunzi watatu, wameuawa eneo la al-Mughayyir mwaka huu, kufuatia ongezeko la ghasia zinazofanywa na walowezi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaodhibitiwa kimabavu. Makazi yote ya walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaodhibitiwa kimabavu ni kinyume cha sheria za kimataifa. Vituo vingi vidogo vya muda vya walowezi vilivyojitokeza kwa wingi karibu na al-Mughayyir pia ni kinyume cha sheria za Israel. Mwalimu Mkuu wa shule ya wavulana ya al-Mughayyir, Bassam al-Assaf, ananiambia: "Wanafunzi wana hofu, na wazazi wao pia wana hofu." Mmoja wa wanafunzi hao, Aws al-Naasan mwenye umri wa miaka 14, alipigwa risasi na kuuawa na mlowezi nje ya lango la shule mwezi Aprili. "Nilikuwa ndani ya darasa langu wakati wanafunzi wawili wadogo walipokimbia kuja kuniambia kuwa kulikuwa na walowezi karibu na ukuta wa shule," anakumbuka mwalimu wa Kiingereza Waheed Abu Naem, ambaye kaka yake Jihad pia aliuawa na askari wa Israel katika shambulio hilo hilo. Waheed anasema alikuwa akijaribu kuwapeleka wanafunzi mahali salama ndani ya lango la shule wakati mlowezi huyo alipowafyatulia risasi. Picha za video zilizochukuliwa kutumia simu ya mkononi zinaonyesha wakati Aws alipopigwa risasi. "Nilipomgeuza na kumweka chali, niliona damu nyingi ikitoka puani na mdomoni mwake, na risasi ikiwa kichwani mwake," anasema Waheed. "Tulimpoteza." Canada yaanza kutoza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa za Marekani Canada imeanza kutekeleza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa mbalimbali kutoka Marekani, huku kukiwa hakuna dalili za nchi hizo mbili kufikia makubaliano ya kibiashara. Ushuru huo unalenga bidhaa za Marekani zenye thamani ya karibu dola bilioni 20, huku viwango vikifikia asilimia 50. Bidhaa zilizoathiriwa ni pamoja na chuma, vifaa vya elektroniki, bidhaa za kilimo na nguo. Canada awali pia ilipanga kutoza ushuru kwa baadhi ya bidhaa za baharini, ikiwemo kamba aina ya lobster, lakini ikaondoa bidhaa hizo baada ya wazalishaji wa sekta hiyo nchini kupinga hatua hiyo. Maafisa wa Marekani na Canada wamesema bado wanataka kufikia makubaliano ya kibiashara, lakini mazungumzo yaliyovunjika mwishoni mwa Agosti hayajaanza tena. Hatua hiyo inaongeza mvutano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, huku Canada ikitegemea kwa kiasi kikubwa soko la Marekani kwa mauzo yake ya nje. Urusi na Korea Kaskazini zafungua daraja la kwanza la barabara kuunganisha nchi hizo Urusi na Korea Kaskazini zimefungua daraja lao la kwanza la barabara linalounganisha nchi hizo, hatua inayorahisisha usafirishaji wa bidhaa na safari za abiria kuvuka mpaka kwenye Mto Tumen. Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimesema daraja hilo litatumika kuwezesha mabadilishano ya wafanyakazi, utalii na biashara. Hata hivyo, shirika la kijasusi la Ukraine, Truth Hounds, limesema daraja hilo limejengwa zaidi kuwa njia ya siri ya kusafirisha vifaa vya kijeshi kwa ajili ya kuisaidia Urusi katika vita vya Ukraine. Ufunguzi huo unafanyika wakati uhusiano kati ya Urusi na Korea Kaskazini ukiendelea kuimarika tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine mwaka 2022. Nchi hizo pia zimesaini makubaliano ya kusaidiana kijeshi endapo mmoja wao atakabiliwa na uchokozi. Waziri Mkuu wa Urusi, Mikhail Mishustin, amelielezea daraja hilo kuwa “ishara mpya ya urafiki”, huku Waziri Mkuu wa Korea Kaskazini, Pak Thae Song, akilitaja kuwa “tukio la kihistoria.” Daraja hilo lenye urefu wa takriban kilomita moja lina njia mbili na lina uwezo wa kupitisha hadi magari 300 kwa siku. Kenya yatoa msamaha wa muda kwa raia wa Afrika Mashariki wasio na nyaraka Serikali ya Kenya imetoa msamaha wa muda kwa raia wa Afrika Mashariki wasio na nyaraka halali, baada ya mamia ya Warundi kufurika katika Ubalozi wa Burundi jijini Nairobi Jumatatu wakitafuta hati za kusafiria, wakihofia kuondolewa nchini kufuatia hatua dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni. Rais wa Kenya, William Ruto, wiki iliyopita aliagiza kufungwa kwa biashara zote ndogo ndogo zinazoendeshwa na raia wa kigeni kuanzia Jumatatu, baada ya kukutana na wafanyabiashara wa Kenya waliokuwa wakipinga marekebisho ya kodi. Wizara ya Biashara ya Kenya baadaye ilifafanua kuwa agizo hilo linawahusu raia wa kigeni wanaofanya biashara bila vibali vya kufanya kazi. Hatua hiyo ilisababisha sintofahamu nje ya Ubalozi wa Burundi Jumatatu, huku baadhi ya Waburundi wakisema walitishiwa na majirani tangu Rais Ruto alipotoa kauli hiyo. Hata hivyo, hakukuwa na dalili za operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao jijini Nairobi Jumatatu. Baadaye, msemaji wa serikali ya Rais Ruto alisema Kenya ina sera ya kutovumilia kabisa aina yoyote ya unyanyasaji, vitisho au ubaguzi dhidi ya wageni. Serikali pia imewataka raia wa Afrika Mashariki wasio na nyaraka halali, hususan Warundi, kujisajili rasmi katika balozi zao. Kenya yaomba radhi kwa Warundi, yaahidi kuwalinda Serikali ya Kenya imewaomba radhi raia wa Burundi wanaoishi nchini humo, baada ya baadhi yao kusema walitishwa au kutendewa vibaya. Hatua hiyo imekuja kufuatia kauli ya Rais wa Kenya, William Ruto, kuhusu raia wa kigeni wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo. Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Korir Sing’Oei, Jumatatu alitembelea Ubalozi wa Burundi jijini Nairobi kuomba msamaha kwa wageni. Sing’Oei amesema uamuzi wa serikali unawalenga raia wa kigeni wanaofanya biashara ndogo ndogo bila vibali, na si raia wote wa kigeni. Amewataka Warundi kubaki watulivu, akisema serikali itaongeza idadi ya maafisa wa usalama katika maeneo yenye idadi kubwa ya Waburundi, yakiwemo Bahati na Muthurwa jijini Nairobi, ili kuwakinga dhidi ya vitisho au unyanyasaji. Ameongeza kuwa wale wanaotaka kubaki Kenya watasaidiwa kujisajili na kupata nyaraka zinazohitajika. Wale wenye vibali vya kufanya biashara wataruhusiwa kuendelea na shughuli zao. Sing’Oei amesema maono ya Kenya ni kuona Waafrika wote, hasa wanaoishi Afrika Mashariki, wakiishi pamoja kama ndugu. Mamia ya Warundi walikuwa wamekusanyika katika ubalozi huo wakiomba hati za kusafiria ili kurejea nchini kwao kutokana na hofu waliyonayo. Pia Unaweza Kusoma; Mbappé ajitosa katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé, amesema anaamini anaweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu. Mbappé, mwenye umri wa miaka 27, amefunga mabao 42 katika mechi 44 akiwa na Real Madrid msimu huu, licha ya kutoshinda taji lolote akiwa na klabu hiyo. Katika Kombe la Dunia, Mbappé alifunga mabao 10 na kutwaa Kiatu cha Dhahabu baada ya kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo. Mbappé pia alivunja rekodi ya ufungaji mabao katika historia ya Kombe la Dunia, akifikisha jumla ya mabao 22. Ufaransa ilimaliza katika nafasi ya nne baada ya kushindwa kufuzu kwa fainali. Akizungumzia nafasi yake ya kushinda Ballon d’Or, Mbappé amesema jina lake limekuwa likitajwa miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo. “Labda mwaka huu ni mwaka mzuri kwangu kushinda tuzo hiyo, lakini wapiga kura huangalia kiwango cha uchezaji,” Mbappé aliwaambia waandishi wa habari. Nyota huyo wa Ufaransa hajawahi kushinda Ballon d’Or. Nafasi yake ya juu zaidi ilikuwa ya tatu mwaka 2023. Miongoni mwa wachezaji wengine wanaotajwa kuwa na nafasi ya kushinda tuzo hiyo mwaka huu ni Harry Kane, Lamine Yamal na Rodri.

How it works

Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.

Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.