Je, Urusi inawaajiri watu wenye ushawishi kutoka nchi za Magharibi ili kuitangaza?
Je, Urusi inawaajiri watu wenye ushawishi kutoka nchi za Magharibi ili kuitangaza?
Mwanaume mwenye ushawishi mitandaoni raia wa Uingereza na Marekani Andrew Tate alichapisha video mapema mwezi Juni akiwa amevaa sare za kijeshi akiendesha kifaru karibu na mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine huku wanajeshi wa Urusi wakiandamana naye.
"Hivi ndivyo tunavyowasha sigara zetu wakati wa kifungua kinywa nchini Urusi," aliandika kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii X, pamoja na video yake akirusha moto (flamethrower).
Machapisho mengine wiki hiyo yalimwonyesha akipiga picha katika Uwanja Red Square huko Moscow na akiinua glasi ya divai kwenye paa ya baa huko Moscow.
Tate, anayekabiliwa na mashtaka ya ubakaji na biashara haramu ya binadamu nchini Uingereza, ni mmoja wa watu wenye ushawishi kutoka nchi ya Magharibi wanaoionyesha Urusi kama mfano mzuri wa nchi.
Maudhui yao yanaonyesha propaganda za Kremlin kuhusu familia, imani ya kidini, na tishio kwa "utamaduni wa Magharibi." Baadhi ya watu hawa wamekaribishwa na maafisa wa Urusi au vikundi vinavyohusiana na serikali.
"Watu wengi hawatawahi kusafiri kwenda Urusi," anasema Helena Ivanov, mtafiti katika Taasisi ya Henry Jackson. "Badala yake, huunda mitazamo yao kulingana na taarifa wanazoziona kwenye mtandao."
Anasema lengo ni kwamba watu wanapofikiria kuhusu Urusi, watafikiria kwanza "makanisa mazuri, maadili ya kitamaduni, ukarimu na urithi wa kitamaduni," si "udhibiti, ukandamizaji wa kisiasa na vita vya Urusi dhidi ya Ukraine."
Mwelekeo huu unakuja huku Moscow ikitafuta njia mpya za kuungana na hadhira ya Magharibi baada ya uvamizi wake nchini Ukraine 2022, jambo lililosababisha vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali kama vile RT na Sputnik kupigwa marufuku kote Ulaya na kufukuzwa kwa wanadiplomasia kadhaa wa Urusi.
Jukwaa dhidi ya Magharibi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Safari ya Tate ilikuwa ni wakati wa Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg, mkutano wa kila mwaka uliowahi kuwavutia Wakurugenzi Wakuu wa Nchi za Magharibi, wawekezaji na viongozi wa kisiasa wenye hamu ya kufanya biashara na kuwekeza nchini Urusi.
Lakini tangu Urusi ilipoanza kuvamia Ukraine, kazi ya jukwaa hilo imebadilika sana. Sasa kwa kiasi kikubwa halihudhuriwi na viongozi na makampuni ya Magharibi, limekuwa jukwaa la upinzani la Urusi dhidi ya ushawishi wa kimataifa unaoongozwa na Magharibi.
Orodha ya wageni wa mwaka huu ilijumuisha safu isiyo ya kawaida ya watu mashuhuri kutoka Marekani, kuanzia mchambuzi wa kihafidhina Candice Owens na Rodney Mims Cook Jr., mwenyekiti wa Tume ya Sanaa ya Marekani, hadi Steven Seagal, mwigizaji na mfuasi wa muda mrefu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Candice Owens, ambaye alizungumza katika mkutano kuhusu maisha ya familia, alitumia safari yake ya kwanza kwenda Urusi kutembelea vivutio vya Moscow na St. Petersburg akiwa na mumewe na watoto, akiweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii.
Katika mahojiano na Rick Sanchez, mtangazaji wa RT na mtangazaji wa zamani wa televisheni wa Marekani ambaye sasa anaishi Moscow, alisema "wanakuambia tu kwamba Urusi ni mahali ambapo hupaswi kwenda."
Cook, ambaye aliteuliwa katika nafasi yake na Donald Trump na ndiye afisa wa kwanza wa serikali ya Marekani kuhudhuria kongamano hilo tangu 2017, alizungumza katika kikao kuhusu "utamaduni" na kusifu "dacha," utamaduni wa kukaa nyumbani wakati wa majira ya joto nchini Urusi.
"Nikiwa Atlanta," aliwaambia wasikilizaji. "Nyumba yangu imejengwa kwa mtindo wa kitamaduni wa usanifu wa mbao wa Urusi, mtindo ambao umekuwa na ushawishi mkubwa kwangu kwa miongo kadhaa," aliongeza.
Maafisa wa Urusi walielezea tukio hilo kama la mafanikio, wakitangaza kwamba zaidi ya watu 24,500 kutoka nchi 142 walishiriki.
Wageni wengi walitoka nchi ambazo zimedumisha uhusiano na Moscow licha ya vikwazo, ikiwa ni pamoja na China, India, na mataifa ya Ghuba.
Ingawa Andrew Tate mwenyewe hakuwepo kwenye jukwaa hilo, safari yake kwenda Urusi ilikosolewa na baadhi ya wanablogu wanaounga mkono vita kwenye Telegram.
Bloga maarufu ya masuala ya kijeshi ya Raibar ilisema, "Sifa yake katika vyombo vya habari iko wazi kwa mtu yeyote mwenye busara: mchochezi anayekabiliwa na mashtaka ya jinai na biashara haramu ya binadamu”.
Kufadhili watu wenye ushawishi
Uchunguzi uliofanywa na vyombo huru vya habari vya Urusi vinavyofanya kazi uhamishoni umebaini mtandao mpana zaidi wa kufadhili maudhui yanayounga mkono Urusi yanayolenga hadhira ya kigeni.
Ripoti za Novaya Gazeta Europe na iStrategy zinaonyesha kuwa RT unafadhili watu wenye ushawishi kutoka nchi za Magharibi kupitia makampuni ya kati baada ya vikwazo vilivyowekwa ambavyo vilisimamisha utangazaji wake katika sehemu kubwa ya Ulaya.
Mara nyingi zikirekodiwa katika maeneo yaleyale ya watalii, video zao zilitengenezwa kwa ajili ya hadhira katika lugha tofauti lakini zilifuata mtindo unaofanana: kuonyesha makanisa, makaburi ya kihistoria, maisha ya familia, na usalama wa umma nchini Urusi, huku zikionyesha taswira ya kuvutia ya nchi kama mahali pazuri pa kuishi.
Baadhi yao pia wameshiriki katika safari zilizopangwa za vyombo vya habari.
Januari 18, 2025, kundi la wanablogu wa kigeni lilitembelea Monasteri Voskresensky nje kidogo ya Moscow, safari ambayo watafiti wanasema iliandaliwa na kituo cha televisheni cha Orthodox cha Urusi Spas, ambacho baadaye kilirusha picha zake.
Jitihada hii inaendana na sera ya Kremlin ya kuvutia wahamiaji kutoka nchi ambazo Moscow inaziita "zisizo rafiki."
Kulingana na sheria iliyosainiwa na Vladimir Putin Agosti 2024, raia wa nchi 47, ikiwa ni pamoja na Marekani, Canada, na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya, wanaweza kuomba makazi ya muda ikiwa watatangaza kufuata "maadili ya kiroho na maadili ya jadi ya Urusi."
Programu hiyo inaungwa mkono na shirika la "Karibu Urusi", ambalo huwasaidia wageni kukaa Urusi.
Shirika hilo lilianzishwa na Mbunge wa Urusi Maria Butina, ambaye alihukumiwa nchini Marekani mwaka 2018 kwa kuwa wakala wa kigeni ambaye hajasajiliwa.
"Shirika hili linawasaidia haswa wale watu ambao wamekumbatia maadili ya Urusi na wanahitaji kimbilio la kiroho na kimaadili," Maria Butina alisema katika mkutano na waandishi wa habari akiwasilisha mpango huo mwaka 2024, kulingana na ripoti ya Kiingereza ya shirika la habari la TASS linaloendeshwa na serikali.
Mmoja wa waanzilishi wa shirika hili ni Martin Held, mjasiriamali wa Austria ambaye anamiliki kampuni ya Urusi ya Fancy Nerd.
Kulingana na iStars, kampuni hiyo ilipokea takriban rubles milioni 45 (karibu dola 600,000) kutoka kwa kampuni mama ya RT, Anno TV Nosti, kupitia makampuni za kati, katika mwaka 2023 na 2024.
Uchunguzi huo huo ulibaini kuwa Alexandra Yost, mmiliki wa chaneli ya YouTube ya "Sasha Meets Russia" kutoka Marekani na Urusi, alipokea hadi dola 2,000 kwa mwezi kutoka RT.
Umoja wa Ulaya ulimwekea vikwazo Juni 2026 kwa kutangaza masimulizi yanayounga mkono Kremlin.
Alexandra Yost anachapisha video za safari kwa wafuasi wake karibu 70,000 kwenye X.
Hukurikodi video katika maeneo kama vile Red Square huko Moscow, miji ya kihistoria ya Golden Ring kaskazini mashariki mwa Moscow, na maonyesho ya ballet ya The Nutcracker.
Chaneli ya YouTube "Real Reporter," inayoendeshwa na mfanyakazi wa zamani wa RT Konstantin Rozhkov, ilizinduliwa kama chaneli ya safari ya lugha ya Kiingereza muda mfupi baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuanza.
Lakini baadaye maudhui yake yalibadilika na kuwa video kuhusu uchumi, vikwazo, na wageni waliosema wamehamia Urusi kwa ajili ya maisha bora.
Jukwaa hilo lilifuta akaunti ya chaneli hiyo mwaka 2025, lakini video za zamani bado zinapatikana kwenye kumbukumbu ya chaneli hiyo, ambayo ina karibu wanachama 500,000.
How it works
Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.
Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.