general237 wordsRead on Arc Codex

Iran yashambulia meli mbili za UAE huku Marekani ikiendeleza mashambulizi

Trump: Mojtaba Khamenei amekufa kwa asilimia 90 Rais wa Marekani Donald Trump ameiambia kituo cha habari cha Fox News kwamba: "Khamenei amekufa, na mwanawe amekufa kwa asilimia 90." Tangu kuanza kwa vita, hakuna picha, sauti, wala video ya Mojtaba Khamenei iliyochapishwa, na hajaonekana hadharani. Siku mbili zilizopita, picha mpya ilichapishwa kwenye tovuti ya Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu, lakini hakukuwa na dalili yoyote inayoonyesha kuwa ilipigwa hivi karibuni. Katika mahojiano na Fox News Rais Trump alisisitiza tena kuwa jeshi la majini, jeshi la anga, na vikosi vya ulinzi vya Iran vimelemazwa na viongozi wake wameuawa. Rais huyo wa Marekani pia alisema kuwa "makubaliano yalifikiwa kuhusu kila kitu" jana baada ya "mkutano wa saa 11," akirejelea suala la Iran. Hakutaja maelezo ya mkutano huo. Aliongeza: "Kazi yao huwa inachukua saa 11 wakati inapaswa kuchukua dakika moja tu... lakini walipotoka chumbani, walipiga simu tena na kusema kuwa kuna mabadiliko yaliyohitajika kufanywa." Donald Trump aliongeza: "Siku zote huwa kuna mabadiliko. Unajua, wao ni wataalamu wa mazungumzo, hiyo ndio kazi yao. Sisemi kwamba wanaimudu vyema kazi hiyo... Hawakupata chochote kutoka kwangu." Bw. Trump alisema siku chache zilizopita kuwa Iran imekubali kila kitu, lakini saa chache baadaye walishambulia meli ya kibiashara katika Mlango-bahari wa Hormuz. Anaituhumu Iran kwa kucheza michezo ya hila dhidi ya marais wa Marekani, akiwemo Bill Clinton, George Bush na Barack Obama, katika kipindi cha miaka 47 iliyopita, huku akimtaja Bw. Obama kuwa "mbaya zaidi kuliko wote." Soma zaidi:

How it works

Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.

Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.