economic_finance5956 wordsRead on Arc Codex

Kesi ya Lissu yaendelea mahakamani

Lissu: Umeeleza hotuba yangu ilikuwa karibu saa mbili na zaidi nilieleza nini? Brenda: Mwenyekiti alikuwa anaeleza matatizo na maeneo ambayo yalihitaji marekebisho nchi inahitaji reforms na kuzungumzia msimamo wetu wa no reforms no election pia nakumbuka akisema bila reforms ni ngumu kupata democratic election na la mwisho nakumbuka hayo maneno ya uasi yalitokana na G55 Lissu: G55 ni nini? majaji hawakueko kwenye mkutano huo. Brenda: G55 ilikuwa ni kikundi cha watu ndani ya chama walitaka kushiriki uchaguzi na walisema no reforms no election inaashiria uasi kwa hiyo mwenye kiti alikuwa anaelezea kwanini ilikuwa ni lazima kupinga uchaguzi usio huru na wa haki. Lissu: Waeleze majaji kuwapo kwa nia ya kuitishia serikali kwenye hiyo hotuba ya saa mbili na nusu. Brenda: Sioni nia ya kuitishia serikali. Lissu: Waeleze majaji umenifahamu kwa muda gani na mimi ni mtu wa aina gani. Brenda: Nimemfahamu Mwenyekiti kama kiongozi kwa miaka 13 kama kiongozi anayepigania demokrasia kama mgombea urais na ninamfahamu kwa mwenyekiti wa chama na mpiganaji aliyeumizwa na serikali ya Tanzania kwa kutokupewa mafao yake ya kibunge kwa kuwa harassed na kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa mahabusu na kutolewa sababu ya misimamo yake ya kupigania haki na demokrasia Tanzania. Lissu: Waeleze majaji huyo mtu uliyemuelezea hivyo ni mhaini kwa nchi yake. Brenda: Inaonesha ni mtu mzalendo na mwenye mapenzi makubwa kwa nchi yake na mtu ambaye anatenda haki ni ngumu yeye kuwa mhaini. Lissu: Nimemaliza waheshimiwa majaji Ahsante. Brenda amemaliza kutoa ushahidi wake wa msingi kinachofuata ni upande wa jamhuri kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyu. Brenda - Nilikamatwa Namanga nikasafirishwa hadi Dar es Salaam Lissu: Waeleeze majaji kitu gani kiliendelea baada ya mkutano wa tarehe tatu baada ya mimi kukamatwa na kufunguliwa mashitaka Brenda: Baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka chama kilifungiwa tarehe 10 mwezi wa sita na baada ya hapo ukaanza ukamataji wa viongozi wa chama na mimi mwenyewe nilikamatwa tarehe 12/07/2025 Namanga border stop nikiwa naelekea Nairobi kwa ajili ya kutembelea ndugu na baadaye niendelea na safari kwenda Ujerumani lakini sikufanikiwa kuvuka ule mpaka. Lissu: Waeleze majaji ulikuwa unaenda Ujerumani kufanya nini Brenda: Nilikuwa ninakwenda kwenye mafunzo ya mawasiliano Lissu: Ilikuwa ni training ya namna gani? Brenda: Kabla chama hakijafunguliwa Katibu Mkuu aliniteua kwenda kwenye mafunzo hayo ya mawasiliano na uongozi Ujerumani na sikufanikiwa na badala yake nilisafirishwa na probox na watu nisiowafahamu wala hawakuwa na sare za polisi kutoka Namanga hadi Longido walikuwa na mwendo mkali sana spidi 120 na zaidi tulipofika Longido wakaniingiza kituoni hawakuruhusu nijiandikishe popote na hawakuniambia kwanini tumesimama hapo hata nilipouliza hakukuwa na majibu zaidi ilikuwa na kutokuelewana kati yangu na wao. Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya hapo? Brenda: Baada ya kupiga kelele sana wakasema wananipeleka Arusha Central wakasema niko salama niko mikononi mwa Polisi. Lissu: Endelea. Brenda: Bado nilikuwa na hofu sababu gari ilikuwa inatembea kwenye spidi kubwa isiyo ya kawaida na niipofika Arusha RPC alikuja kuonana na mimi nje ya kituo kwenye maegesho ya magari alijitambulisha kama RPC sikumbuki jina hapo. RPC huyo alitukabidhi gari nyingine kubwa kama VX lenye namba plate ya zanzibar wakaongezeka pia wanaume wawili wakasema tunaelekea Dar es Salaam na hiyo ilikuwa saa nne usiku. Jaji: Ndio. Brenda: Hii gari ilikuwa inatembea spidi kubwa na kila tuliposimamishwa walikuwa wanasema ni kazi maalumu na tunaruhusiwa kupita. Lissu: Mnasimamishwa na nani? Brenda: Tulikuwa tunasimamishwa na polisi wa barabarani kwenye check point walisema kazi maalum. Lissu: Mlifika Dar saa ngapi? Brenda: Saa kumi kamili tukafikia kituo cha polisi Oysterbay na wakatuambia twende central huko tulipofika wakampigia George Bagemi akasema anakuja. Lissu: Hiyo ilikuwa saa ngapi? Brenda: George alifika saa kumi na moja na nusu Central Lissu: Baada ya Deputy ZCO George Bagemi kufika nini kilifuata? Brenda: Neno lake la kwanza lilikuwa nilikuwa nakusubiri nitakuweka ndani kisha akaniambia wamenikamata sababu ya taarifa ambayo nilitoa kwa Umma tarehe 2 julai 2025. Lissu: Hiyo taarifa kwa umma ilikuwa inahusu kitu gani? Brenda: Hiyo taarifa kwa Umma inahusiana na mbunge wa bunge la Ulaya na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje kwenye Bunge la EU David Macalister kuhusiana na ripoti ya kwamba kuna mpango wa kumpa simu mwenyekiti akiwa gerezani. George Bagemi akakabidhiwa simu yangu na passport yangu yenye namba TAE 481364 ambayo mpaka leo hii sijawahi kurudishiwa passport yangu wala simu yangu. Lissu: Taratibu majaji wanaandika. Brenda: Baada ya hapo wakaniambia wanaenda kunipekua nyumbani Basihaya nikiwa kwenye karandinga ya polisi yale magari ya polisi ambayo yako wazi. Lissu: Walipofika kwako kitu gani kilitokea? Brenda: Walipekua kila chumba nguo zote hawakuniambia wanatafuta nini na hawakukuta hicho walichokua wanatafuta. Lissu: Walikuwa na search warranty au search order? Brenda: Sikumbuki nilikuwa na stress na it was very hostile. Lissu: Baada ya hapo Brenda: Tulirudi central, niliwekwa mahabusu kuanzia saa nne na nusu hadi lunch time na nilikaa mahabusu kwa siku nne na sikupewa mashtaka wala kufikishwa mahakamani. Lissu: Kisha nini kilifuata na ulikaa kizuizini kwa jumla ya siku ngapi tangu Namanga? Brenda: Kwa ninavyokumbuka ilikuwa siku nne na nusu niliachiwa tarehe 15. Lissu: Umewahi kushitakiwa? Brenda: Mpaka leo sijawahi kushitakiwa. Lissu: Kwa wewe kutoa hiyo taarifa ya Mbunge wa Ulaya wewe ulitenda kosa gani? Brenda: Sikuambiwa ni kosa hata niliposhikiliwa. Lissu: Tuendelee. Brenda: Wakati nakamatwa mtaalamu wa rasilimali wa chama naye alikamatwa airport Leonard Magere na baadae Amani Golugwa na hakuna yeyote kati yetu aliyefunguliwa kesi mahakamani Ushahidi kuhusu kesi ya Lissu unaendelea Alidai kuwa yeye alikuwepo wakati wa mkutano huo Aprili 3, 2025 Alidai mzungumzaji mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu. Alidai kuwa kwa kumbukumbu zake, mkutano huo ilichukua takribani saa tatu nusu. Alidai kwa kumbukumbu zake, mzungumzaji mkuu alizungumza kwa kipindi kirefu kuliko wazungumzaji wote. Lissu: Katika mkutano huo, mimi nimetengeneza nia na kuitisha Serikali. Alidai hukutengeneza nia, wala kuitishia Serikali na wala hakuna uwepo wa Serikali kwenye maneno yako. Alidai katika maeneo aliyosoma hakuna uwepo wa neno makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano. Pia katika maneno aliyosomewa na mshtakiwa hakuna uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala Baraza la mawaziri wa Jamhuri ya Muungano. Vile alidai hakuna uwepo wa neno Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania, wala Halmashauri ya Jiji. Vilevile hakuna uwepo wa neno Waziri, Naibu Waziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri au Kiongozi yoyote wa Kiserikali. Alidai kuwa maneno aliyosomewa na mshtakiwa ambayo ni hati ya mashtaka hayatishi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia katika maneno aliyosomewa na mshtakiwa, shahidi alidai hakuna neno lolote linalohusu Jeshi lolote liwe Jwtz, Magereza, Jeshi la Polisi Mgambo, Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, Jeshi la akiba. Pia hakuna neno wakachome vituo vya daladala, mwendokasi, wala kateni watu vidole. Lissu: Kuna maneno yamesemwa hapa, kuwa Polisi 16 waliuawa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Sasa waeleze majaji kama katika maneno yangu nilisema tutaenda kuua Polisi. Shahidi: Hayapo.Alidai kuwa Kwa ufahamu wake kuwa mtu akisema msimamo huu unaashiria uasi, hilo sio kosa. Pia alidai Kwa ufahamu wake sio kosa kuwa mtu akisema watazuia uchaguzi. Vilevile kwa ufahamu wake, mtu akisema tutauvuruga uchaguzi anakuwa hajatenda kosa lolote. Alidai kuwa hajaona video iliyooneshwa na jambo Tv, ikichezwa na kuoneshwa mahakamani. Pia hajaona video yenye maneno machache ambayo yapo kwenye hati ya mashtaka. Alidai zaidi ya maneno ya mashahidi yaliyotokea mahakamani, hakuna ushahidi wa video ulitolewa mahakamani hapo. Alidai kuwa mshtakiwa Tundu Lissu sio mfanyakazi wa Jambo Tv na wala hajapeleka video inayodai kuchapisha Jambo Tv. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu 08.9.2026 Lissu: Waeleze majajji nani aliyeamua huo mkutano ufanyike Brenda ni shahidi mwengine wa upande wa Tundu Lissu Lissu: Nje ya hizi nafasi za kichama wewe ni nani Brenda: Mimi nimesomea Bachelor of science in Accounting Gloucestershire University nchni Uingereza kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2013 Lissu: Waeleze majaji Tuzo au awards uliyoipata baada ya kusoma huko Brenda: Nilipata Cheti baada ya kuhitimu Lissu: Waeleze majaji utaalamu wako mwingine kama upo Brenda: Hapana hakuna Lissu: Waeleze majaji uzoefu wako wa kazi za kitaaluma nje ya kazi za kisiasa Brenda: Kwa mwaka mmoja baada ya kuhitimu nilifanya kazi kwa mwaka mmoja na baadae nikaanza kufanya biashara za kawaida Lissu: Waeleze majaji ulifanya kazi gani wapi na mwaka gani Brenda: Niliajiriwa kama accountant TAZ Cars nilifanya kwa mwaka mmoja nikaanza kufanya biashara Kariakoo Lissu: Ulifanya kazi kwenye hiyo kampuni toka lini hadi lini Brenda: Nilipohitimu mwaka 2013 niliajiriwa mpaka mwaka 2015 na baada ya hapo nikaanza kufanya biashara ya nywele na urembo wa wanawake Kariakoo na baadaye nikaanza kuuza vifaa vya umeme Lissu: Ukisema uliuza urembo una maaana gani? Brenda: Nilikuwa nauza vifaa vya urembo Lissu: Sasa shahidi baada ya kutupa historia yako kwa ufupi naomba tuzungumzie kesi ambayo unaitolea ushahidi leo hii. Swali langu la kwanza kuhusiana na hii kesi waeleze majaji ufahamu wako juu ya mkutano wa tarehe tatu April 2025 Brenda: Waheshimiwa majaji Chama kilialika watia nia makao makuu ya chama mikocheni kuja kuzungumzia kuhusiana na msimamo wa ‘No reforms no election’ Lissu: Waeleeze majaji hao watia nia ni watu gani Brenda: Ni wale waliokuwa na nia kugombea chaguzi za kiserikali 2025 Lissu: Waeleze majaji hiyo uliyokuja kuzungumzia ‘No reforms no election ni nini Brenda: Ni msimamo wa chama ulioelekeza bila mabadiliko hakuna uchaguzi mabadiliko ya sheria za kiuchaguzi Lissu: Waeleze majajji nani aliyeamua huo mkutano ufanyike Brenda: Ni katibu mkuu wa chama na sekretarieti Lissu: Katibu mkuu ni nani? Brenda: Waheshimiwa majaji katibu mkuu anaitwa John Mnyika Lissu: Unaposema sekretarieti una maana gani shahidi Brenda: Ni chombo cha utekelezaji wa kazi za chama za kila siku Lissu: Hiki chombo kina wajumuisha wakina nani? Brenda: Waheshimiwa majaji hiki chombo kinaundwa na katibu mkuu na manaibu wake wawili wa bara na Zanzibar Mkurugenzi wa chama Lissu: Hao manaibu katibu hawana majina Brenda: Mmoja anaitwa Amani Golugwa bara na wa Zanzibar anaitwa Ally Ibrahim Wakurgenzi ni Brenda Rupia mkurugenzi mawasiliano na uenezi, John Kitoka mkurugenzi mambo ya nje, Mkurugenzi wa Fedha Tito Kitalika, Mkurugenzi wa operesheni na uchaguzi John Pambalu, Mtaalamu wa rasilimali Lenard Magere, Makatibu wa mabaraza , Baraza la wazee Hellen Kayanza, Baraza la wanawake Pamela Maasai, Baraza la vijana Dua Lyamzito, Mkurugenzi wa sheria Gaston Galubindi. Lissu: Waeleze majaji huo mkutano wa sekretarieti ulifanyika lini? Brenda: Sikumbuki tarehe ya kikao tulichofanya ili kuitisha huo mkutano Lissu: Sasa waeleze waheshimiwa majaji kikao hicho kiliamua nini kifanyike Brenda: Waheshimiwa majaji kikao hicho kiliamua kwamba tutoe taarifa kwa watia nia kwenye huo mkutano na kwamba Chadema itakuwa na watia nia kwenye huo mkutano Lissu: Baada ya kuamua watia nia wafahamishe na umma ufahmishwe kitu gani kilifanyika Brenda: Mkurugenzi wa mawasiliano aliandika ujumbe kwa umma tarehe 27/03/2025 kuujulisha umma kutakuwa na mkutano na watia nia tarehe tatu April na kuwataka watia nia wafike ofisi za chama kwa ajili ya mkutano huo na chama. Lissu: Nini kilifuata Brenda: Tuliweka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii baada ya kuwa nimeandika kwa kurugenzi yangu ya mawasiliano ambayo ilitoa taarifa juu ya mkutano huo kwa vyombo vya habari na nikavialika Lissu: Naomba urudie tena Brenda: Niliandika barua nikaweka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za Chama, Kisha nikaalika vyombo vya habari Lissu: Sasa mimi nimeshitakiwa na nimekuwa gerezani nikituhumiwa mimi ndiye niliyealika vyombo vya Habari, wewe unasemaje? Brenda: Waheshimiwa majaji Mheshimiwa Tundu Lissu sio yeye aliyeandaa mkutano na watia nia wala kualika vyombo vya habari Lissu: Waeleze majaji kwenye mwaliko wa waandishi wa habari iwapo kulikuwa na maelekezo yoyote waje na nini na waje wafanye kazi yao vipi Brenda: Tunapowaalika waandishi wa habari hatuwapi maelekezo yoyotewanakuja kufanya kazi yao kwa utaalamu wao, na tuliwaalika waje wachukue taarifa ya watia nia na chama Lissu: Waeleze majaji siku ya mkutano watu gani walihudhuria mkutano huo Brenda: Waheshimiwa majaji watia nia walihudhuria, wajumbe wa sekretarieti pamoja na viongozi wakuu wa Chama Lissu: Viongozi wakuu wa chama ni akina nani Brenda: Viongozi wakuu wa chama ni Manaibu makatibu wakuu wawili Aman Golugwa na Ally Ibrahim, Makamu mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Makamu, mwenyekiti Bara Mheshimiwa John Heche na Mwenyekiti Taifa Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu na katibu mkuu wa Chama Mheshimiwa John Mnyika. Lissu: Watu gani wengine walikuepo? Brenda: Walikuepo watia nia wa sekretarieti pamoja na waandishi wa habari Lissu: Ulikuwa na wastani wa watu wangapi? Brenda: Takribani watu 250 Lissu: Waeleze majaji kimahususi kuhusiana na waandishi wa habari waliokuja ni wa vyombo gani vya habari Brenda: Waandishi waliokuja ni pamoja na Chanzo TV Mwanzo TV, Jambo TV, ITV na vyombo vingine vya online ikiwemo Mwananchi, hao ndio ninaowakumbuka Lissu: Walikuja vipi? Brenda: Waheshimiwa majaji walikuja na kamera na vipaza sauti na wengine kalamu na karatasi Lissu: Sasa ushahidi umeletwa mahakamani, kati ya hao waandishi wa habari waliokuja, wapo waliorusha matangazo ya mkutano huo moja kwa moja waeleze majaji moja kwa moja Brenda: Ni ngumu kesema kama walirusha au hawakurusha sababu kuna wanaorekodi na kurusha baadaye na kuna ambao hawatarusha kabisa Lissu: Kuna taarifa kwamba Jambo TV walirusha Taarifa hiyo moja kwa moja, wewe unasemaje? Brenda: Waheshimiwa majaji ni ngumu kusema sababu hatuwapangii namna ya kufanya kazi Lissu: Wewe ulikuwepo kwenye huo mkutano uliona wakifanyaje kazi? Brenda: Waheshimiwa majaji, waandishi walikuwepo ila ni ngumu kusema kama walirusha matangazo moja kwa moja au la au hata kama walirekodi sababu walikuwa tu kwenye huo mkutano Lissu: Kwa kuwa mimi ndio mshitakiwa waeleze majaji mimi nilifanya nini kwenye mkutano huo Brenda: Mwenyekiti alikuwa mzungumzaji pamoja viongozi wengine wa chama Lissu: Nilikuwa mzungumzaji wa aina gani? Brenda: Hapana ulikuwa mzungumzaji mwalikwa na ulitoa hotuba kama mwenyekiti wa chama na ndio alikuwa mzungumzaji mkuu Lissu: Waeleze majaji kitu kingine chochote ulichokiona mwenyekiti akifanya zaidi ya kuwa mzungumzaji mkuu Brenda: Sikuona kitu kingine chochote mwenyekiti alichokifanya zaidi ya kuwa mzungumzaji mkuu Lissu: Ushahdi uliopo unasema mimi ndiye niliyetayarisha hayo matangazo na kuyaweka mitandaoni hususan jambo tv wewe unasemaje? Brenda: Waheshimiwa majaji hayo yatakuwa mashitaka ya uongo na wala sio mfanyakazi wa jambo tv hayo ni mashitaka ya uongo na wala alikuwa hafahamu kama Jambo tv watakuepo kwenye huo mkutano Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji Nzengelei waheshimiwa majaji tunaona muda umekwisha tunaomba muongozo wa mahakama kama shauri linaweza kuahirishwa Jaji: Tuendelee kidogo Lissu: Ahsante waheshimiwa nimalizie hili. Shahidi swali langu lilikuwa mwenyekiti hakuwa anajua juu ya uwepo wa jambo TV waeleze majaji mwenyekiti kufahamu kama anajua waandishi wa habari walikuwa wamealikwa Brenda: Sinadhani kama alikuwa anafahamu, sababu ni kazi yangu mimi na kurugenzi ya mawasiliano Lissu: Swali langu la mwisho kwa leo nani ni mmiliki wa hayo matangazo au hiyo Taarifa. Brenda: Ni Mmiliki wa chombo husika Lissu: Waeleze majaji kuhusu Taarifa iliopeperushwa na Jambo tv April tatu mwaka jana Brenda: Waheshimiwa majaji mmiliki wa taarifa ya Jambo TV ni jambo TV wenyewe au mkurugenzi wa Jambo TV Jaji: Shauri linaahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi Lissu amuhoji Mkurugenzi wa Mawasiliano CHADEMA Lissu: Shahidi wangu namba nne anaitwa Brenda Jonas Rupia Jaji: Shahidi unaitwa nani? Brenda: Naitwa Brenda Jonas Rupia Mkurugenzi wa Mawasiliano na uenezi CHADEMA Shahidi anakula kiapo Lissu: Umesema unaishi Basihaya kata ya Bunju iko wapi? Brenda: Waheshimiwa majaji Basiaya iko ndani ya jimbo la Kawe wilaya ya Kindondoni Mkoa wa Dar es salaam Lissu: Umewaeleza majaji wewe ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi CHADEMA hii kazi umefanya tangu lini? Brenda: Kuanzia tarehe 12/3/2025 nilipoteuliwa na kamati kuu ya chama Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kabla ya hiyo tarehe ulikuwa na nafasi gani ndani ya Chama Brenda: Nilikuwa katibu wa Bawacha Mkoa wa kichama Kindondoni Lissu: Waeleze majaji Bawacha ni nini Brenda: Waheshimiwa majaji Bawacha ni Baraza la wanawake CHADEMA Lissu: Hiyo nafasi ya Bawacha ulishapata hiyo nafasi tangu lini? Brenda: Nilishika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja nikiteuliwa mwaka 2024 Lissu: Waeleze majaji nafasi nyingine uliyokuwa nayo ulipochaguliwa Kinondoni Brenda: Nimekuwa mwenyekiti CHADEMA kata ya Mwananyamala na baadaye nikachaguliwa mwenyekiti wa Bawacha jimbo la kinondoni vyote hivyo ni kati ya 2015 na 2024 Shahidi anayefuata ni Brenda Rupia Mahakama imerejea Shahidi: Ilikuwa haki yetu kushiriki uchaguzi huru na wa haki lakini tulizuiliwa Lissu: Sasa shahidi nilisema ilikuwa haki yetu kutoshiriki uchaguzi ila tulizuiliwa na tume ya uchaguzi hebu fafanua Shahidi: Ni kweli ilikuwa haki yetu kushiriki uchaguzi huru na wa haki lakini tulizuiliwa na tume ya uchaguzi Lissu: Unakumbuka kutoa ushahidi kuhusiana na kuenguliwa kwa wagombea wa CHADEMA ukasema hujawahi kuona uchaguzi wowote huru ulioendeshwa na Tume ya Uchaguzi ukaulizwa kama CCM walisema wagombea wao wameenguliwa fafanua Shahidi: Taarifa za wagombea kuenguliwa zinakuweko kwenye ofisi za taasisi na sijawahi pokea taarifa yoyote kutoka Chama cha Mapinduzi Lissu: Uliulizwa juu ya usahihi wa mahesabu yako juu ya matokeo ya rais ukasema asilimia 98.6 zilienda kwa Samia ukasema asilimia mbili nukta nne zilienda kwa wengine. Ulipoulizwa kama unajua hesabu ulisema hiyo ni human error ulikuwa na maana gani? Shahidi: Waheshimiwa …… Jaji: Si ni human error aseme nini kingine Lissu: Inatosha hiyo kaka Shahidi: Inatosha Lissu: Uliulizwa kama maandamano huleta bugudha kwa watu ukasema maandamno huleta bugudha kwa watu fulani hebu fafanua jibu lako Shahidi: Ni kweli inaleta bugudha kwa watu mbali mbali, huwa ni bugudha inayowasha masikio na macho. Utaratibu wa siku huwa unabugudhika kwenye barabara Lissu: Shahidi uliulizwa maswali mengi kuhusu uhuru wa Tanzania ukasema ndio na mahakama hazitakiwi kuingiliwa na taasisi nyingine za nje. Ukaulizwa kama zinaweza kuelekezwa na EU lakini mamlaka nyingine zinaweza zungumzia maswala ya ndani ya Tanzania ikiwepo masuala yaliyoko mahakamani ulikuwa na maana gani? Shahidi: Tanzania sio kisiwa kama nchi ina wajibu wa kuzingatia matamko ya kidunia yanayohusiana na haki za binadamu inawajibika kuheshimu sheria za kimataifa Wakili: Huu ni ushahidi mpya waheshimiwa majaji naona wanaanza kuleta mambo mapya waheshimiwa majaji Lissu: Ulisema mtu mmoja peke yake hawezi akafanya kosa la uhaini fafanua Shahidi: Nilichomaanisha mshitakiwa hawezi kutenda kosa la uhaini peke yake kwamba amepanga yeye akachochea baada ya kujichochea na kufanya hilo kosa mwenyewe Lissu: Uliulizwa juu ya uhuru wa tume na ukasema huo uhuru wa tume haupo sababu huo uteuzi umelenga kuweka udhibiti kwa mtu mmoja ulikuwa na maana gani Shahidi: Uteuzi huwa unafanywa na mtu mmoja ambaye ni rais na wale aliowateua na kwamba wanampa yeye kipaumbele Lissu: Uliulizwa mwaliko kwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ilikuwaje umualike wakati yeye ni sehemu ya kamati ya maandalizi na ukasema ilikuwa tu nia njema sababu anaishi Zanzibar Shahidi: Waheshimiwa majaji Jaji: Unamajibu tofauti Shahidi: Ni hayo hayo tu waheshimiwa majaji Lissu: Unakumbuka uliulizwa maswali mengi kuhusina na mkutano wa Aprili ulinikatisha kwenye mkutano ila hukuniandikia hotuba wala hukunipa hotuba ila ulijua nini kiko kwenye fikra zangu ziku hiyo Shahidi: Nilichomaanisha ni kwamba sekretariet inapoandaa mkutano nilikuwa ninajua tunazungumzia swala la ‘no reforms no election’ Lissu: Uliulizwa juu ya mikutano ambayo mimi na wewe tulifanya na wadau mbalimbali, uliulizwa mkutano wetu na Shura ya Maimam, ukaulizwa kama yale maneno ya kuzuia uchaguzi kama niliyasema, ukaulizwa kama nilisema kukinukisha kwa Warioba na punde ukasema sikusema ukaulizwa huoni unatoa ushahidi wa uongo ulikuwa na maana gani Shahidi: Nilikuwa namaanisha ni hali ya kawaida ya mtiririko wa mazungumzo, muktadha wa jambo la msingi huwa linasema kwa hiyo hilo neno moja kukosekana halikuondoa maana ya ujumbe husika kufikishwa Lissu: Leo umeulizwa na Katuga zile rekodi zinazochukuliwa na chombo cha habari ni mali ya chombo husika ukasema ni mali yake kwa chombo husika ukaulizwa useme kifungu ukasema hujui hebu fafanua Shahidi: Kwa ninavyofahamu anayerekodi ndiye mwenye kile kinachorekodiwa sababu yeye amekuja na vifaa vyake Lissu: Umeulizwa nilisema majaji ni Ma-CCM ukasema hukumbuki na ukaulizwa kama nikisema mahakamani hakuendeki na mapolisi wanaingiza kura kwa vibegi. ukasema hukumbuki ulimanisha nini? Shahidi: Nilimaanisha kile nilichokisema kilitokana na kile nilichokisikia Lissu: Uliulizwa juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ukasema kweli kulikuwa na vurugu ukasema jumuiya ya Ulaya ilisikitishwa na vurugu hizo na ukasema sio kweli kwamba Lissu ndio alisababisha vurugu sababu alikuwa gerezani Shahidi: Nilichokuwa namaanisha hapo baada ya CHADEMA kuzuiwa kufanya shughuli zake haikujihusisha na siasa tena na mwenyekiti alikuwa gerezani na sio kweli kwamba vurugu zilizotokea zililetwa na CHADEMA au nini Lissu: Uliulizwa kuhusu hotuba ya jaji Chande ukasema ulisikiliza sehemu sehemu ukasema alisema vurugu za Oktoba zilipangwa ukasema hukumbuki. Ukaulizwa uchaguzi kuvurugika ukasema uchaguzi ukivurugika na ukasema walioko madarakani wanaendelea ulikuwa na maana gani? Shahidi: Waheshimiwa majaji nilikuwa na maana mbili katiba yetu inatupa fursa ya kusogeza chaguzi mbele kukiwa na changamoto maana ya pili ni maana iliyoko katika msimamo huu ya kwamba tuko tayari. CHADEMA ilikuwa tayari na iko tayari hata ingebidi uchaguzi kusogezwa mbele ili kupata mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi Lissu: Uliulizwa kuhusu kuhamasisha uasi ulisema yanapaswa kutafsiriwa kwa muktadha wake na yangewatia wasiwasi una maana gani? Shahidi: Nilimaanisha mkutano huo wa watia nia walielimishwa kwa kuoneshwa sheria ambazo tunazo na ni mbovu na zinatakiwa kufanyiwa mabadiliko na neno uasi nilimaanisha tutakwenda kinyume na sheria mbovu ili kupata sheria nzuri. Jaji: Shahidi umemaliza kutoa ushahudi wako mahakama inakuruhusu Tunakwenda mapumziko hadi saa tisa 'Unafahamu mshtakiwa anashtakiwa kwa kuvuruga uchaguzi'? Wakili: Ni ushahidi wako unasema Jumuiya ya Ulaya walisikitishwa na vurugu siku ya uchaguzi Shahid: Ni kweli. Wakili: Na pia Mwenyekiti alisema kuwa huu uchaguzi tunakwenda Kuuvuruga Shahidi: Ndio Wakili: Waambie majaji ni kweli au Sio kweli Siku ya Uchaguzi kulikiwa na Vurugu Shahidi: Ni kweli kulikuwa na vurugu Wakili: Nitakuwa sahihi nikisema kile mwenyekiti alichosema kuwa Watavuruga Uchaguzi na kweli Vurugu Zikatokea kwa mujibu wa hotuba ya Mwenyekiti ni kweli au sio kweli kwamba kilichopangwa kwa vurugu kilitumia vurugu zilizotokea Shahidi: Sio kweli Wakili: Unajua au hujui ni aina gani ya Uhaini ambayo ameshtakiwa nayo mshtakiwa unayemtetea Shahidi: Hafahamu Wakili: Je unafahamu au haufahamu mwenyekiti anashtakiwa na aina gani ya shtaka la Uhaini?. Shahidi. Wakili: Unafahamu au haufahamu kwamba mshtakiwa anashtakiwa kwa kuchapisha na kutoa maneno ya Kuvuruga Uchaguzi. Tunakwenda kuzuia huu Uchaguzi na Tunakwenda kukinukisha Shahidi: Anafahamu Wakili: Kwa Mujibu wa ushahidi wako ni kweli au sio kwelikwamba mshtakiwa ametoa hayo maneno Shahidi: Mshtakiwa alitoa hotuba ndefu yenye hayo maneno Wakili: Waambie majaji katika mkutano wa April 3 mwaka 2025 baada ya malalamiko ya upungufu katika Uchaguzi. Mshtakiwa au Mwenyekiti alikuja na alitangaza maadhimio yenye Senstesi Chache zenye nguvu Kwamba Tunaenda Kuzuia Uchaguzi Shahidi: Hawakuwa na kikao chenye maazimio. Wakili: Baada ya Mwenyekiti kusema majaji ni Maccmmahakamani hakuendeki Kilichobaki tuende tukavuruge Uchaguzi na tukazuie Uchaguzi na tunakwenda Kukinukisha ni kweli au sio wajumbe walicheka na kushangilia Shahidi: Hakumbuki Wakili: Umesema kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria na sio haki kumzuia mtu.. je kulikuwa na nia yoyote ya Mwenyekiti Kufungua Kesi mahakamani Kupinga Uchaguzi Shahidi: Hakukuwa na nia ya kufungua kesi kuzuia Uchaguzi bali ilikiwa nia ya kuelimisha Wakili:Je wambie majaji kama ulisema katika Ushahidi wakoMwenyekiti aliwapa katika hotuba yake njia ya kuzuia Uchaguzi Wakili: Huyu unayemzunguzia amesema maneno ‘majaji ni Maccm’ anasema Kayasema kwenye mkutano Je, unakubaliana naye? Shahidi: Hajawahi kuyasikia hayo maneno Wakili: Waambie majaji kama vikao vya chama chenu huwa vinakuwa na maazimio Shahidi: Katika utaratibu wa kawaida vikao vinakuwa na Maazimio 'Ni kweli au sio kweli kwamba neno kukinukisha ni kitendo'? Wakili: Waambie majaji ni kweli au sio kweli katika uandishi wa kumbukumbuku za maazimio ni yenye sentesi fupi zenye kueleweka. Shahidi: Ni kweli Wakili: Neno kukinukisha uliliskia?. Shahidi: Ndio nilisikia. Wakili: Ni kweli au sio kweli kwamba neno kukinukisha ni kitendo Shahidi:. Ni kitendo Wakili: Katika ushahidi wako ulioeleza mahakama ni kitendo gani kilisemwa na mwenyekiti ili kukinukisha kufanyike Shahidi: Hakusema kitendo bali alitoa tafsiri ya neno kukinukisha Wakili: Waambie majaji ukichoma kitu ikiwemo matairi yanatoa au hayatoi harufu Shahid: Hakumbuki Wakili: Je mwenyekiti siku ya hotuba yake alieleza njia ambayo itatumika kukinukisha katika Uchaguzi Mkuu... Shahidi: Haikueleza hiyo dhamira. Wakili: Inawezekana watu waliambiwa kama mashabiki wa simba wakachimbe Jangwani dawa Shahidi:… Wakili: Ni haki au sio haki kwa mtu yeyote aliyepo kusikiliza hotuba ya Lissu na kutafsiri yale maneno kwa jinsi anavyojua yeye Shahidi: Siwezi jisemea. Wakili: Kwa kuwa njia ya kukinukisha haikuwa imefafanuliwa nitakuwa sahihi nikisema ni haki ya mtu akiamua kwenda kujisaidia kwenye kituo cha kupiga kura na kuacha dude lake pale linanuka. Shahidi: Sio Haki Wakili: Waambie majaji ni haki au sio haki kwa hiyo mtoaji wa hiyo hotuba kwenda kufanya vituo vya kupiga Kura vinuke kwa kuchoma moto ''Sentensi 'Tunaenda kuzuia uchaguzi' ni kamilifu na yenye maana?'' Wakili: Waambie majaji iwapo sentensi TUNAENDA KUZUIA UCHAGUZI ni kamilifu na yenye maana au sio kamilifu isiyo na maana Shahidi: Ni kamilifu na ina maana Wakili: Unaenda kuvuruga uchaguzi Je, ni Kamilifu na inayotoa maana au sio kamilifu na isiyoleta maana. Shahidi: Ni kamilifu ukisoma yote Wakili: Ulirejelea hotuba ya mwenyekiti ya Aprili 3, ulirejelea maneno mengi sana na uliwaambia majaji kuwa kilichoandikwa kwenye hati ya mashtaka ni kisehemu kidogo chenye sekunde 26. Sasa waambie majaji kwenye hiyo hotuba kama ulisikia kweli, je ulimsikia mwenyekiti akisema kwamba majaji ni MACCM? Shahidi: Hakumbuki. Wakili: Je ulisikia mahakamani hakuendeki Shahidi: Hakumbuki Wakili: Je, ulisikia mwenyekiti akisema kuwa mapolisi wanaingiza kura feki kwenye vibegi vya mgongoni Shahidi: Hakumbuki Wakili: Wewe yale uliyoyasema ukirejea maneno ya mwenyekiti kwenye mkutano wa mwenyekiti wa Aprili 3 mwaka 2025 umeyasema yote au machache kati ya mengi aliyoyasema Shahidi: Nimesema yale katika yote aliyoyasikia yeye. Wakili: Je, hujui au unajua kama yapo maneno mengine ambayo alisema ambayo wewe huyajui. Shahidi: Sifahamu Wakili: Je yale uliyoyasema hapa mahakamani yamechukua Lisaa moja na Nusu au yamechukua Dakika Chache Shahidi: Yale ambayo ameyasema Shahidi Aman Golugwa anaendelea kuhojiwa KATUGA. Wakili: Waambie majaji ni kwelii kwamba aliwaambia vile vitu vilivyochukuliwa na mwandishi wa habari ni mali yake na anaweza kutumia atakavyo Shahidi: Ni kweli Wakili: Hayo maneno ni kwa mujibu wa sheria au kwa mujibu wa maoni yako Shahidi: Ni kwa mujibu wa sheri na uelewa wake Wakili:Je, umetaja sheria gani, je katika ushahidi wako umeitaja Sheria Mahususi Shahidi: Ni mali yake na kwamba hajataja Sheria. Wakili: Ni kweli kuwa nilikusikia kwamba uliwaambia Majaji kuhamasisha uasi sio kosa kisheri ni neno La kisiasa Je, unakumbuka ulisema haya maneno? Shahidi: Ndio nakumbuka kuyasema Wakili: Je, siasa mnazofanya mnatumia lugha gani Shahidi: Lugha ya Kiswahili. Wakili: Kamusi gani inayotumika kutafsiri hiyo Lugha ya Kiswahili Shahidi: Wanatumia kamusi ya Kiswahili kutafsiri. Wakili: Je, kwa ufahamu wako kuna kamusi inayoitwa kamusi ya Lugha ya Kisiasa. Shahidi: Hakuna kamusi ya Lugha ya kisiasa Wakili: Ulikuwa unarejeshwa kwenye maneno ya hati ya mashtaka ulisema kwa ufahamu wake unaotokana na uzoefu wa siasa hakuna kosa lolote mtu akisema anaenda kuvuruga Uchaguzi hii ni kwa mujibu wa sheria au uzoefu wako? Shahidi: Sio maoni ni kweli kwa shughuli za Kisiasa Wakili: Je, unajua au hujui kuwa uchaguzi mkuu upo kwa mjibu wa katiba Shahidi: Anafahamu kuwa uchaguzi Mkuu wa Wabunge madiwani na Rais upo kwa mujibu wa katiba Wakili: Ulimwambia jaji kwa ufahamu wako kwamba kitendo cha kuvunja sheria hakikupeleki kuwa na kosa la Uhaini Shahadi: Hadi akumbuke Wakili: Ulisema kitendo cha kupinga sio kosa je, Ulitaja Sheria Shahidi: Kupinga sio kosa ila sikutaja Sheria. Natumai hujambo na karibu tena katika muendelezo wa habari za moja kwa moja kutoka mahakamani Katuga kwa Golugwa- Ulisema mpaka mshinikize mabadiliko mumshinikize nani? Katuga: Wewe ni miongoni mwa watu wanaotaka katiba ya nchi ibadilishwe unaifahamu vizuri? Golugwa: Ndio ila sio yote kwa kuisoma. Katuga: Kama nilikusikia vyema umezungumza sana ushenzi ushenzi nitakuwa sahihi nikisema wewe ni shahidi wa ushenzi. Golugwa: Sio sahihi Katuga: Waambie waheshimiwa majaji kabla ya kuwa naibu katibu mkuu ulikuwa katibu mkuu kanda ya kaskazini Golugwa: Katibu wa kanda. Katuga: Ni kweli ulieleza mahakama kuwa uliandaa taarifa kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Golugwa: Ni kweli. Katuga: Ni kweli kwamba kwenye taarifa yako uliandika maneno makali kwa ushenzi huu ulisema mpaka mshinikize mabadiliko mumshinikize nani? Golugwa: Ni kweli na ilikuwa kushinikiza mamlaka husika. Katuga: Waambie majaji kama unajua au hujui mtu yoyote akitoa hoja jukumu la kuithibitisha hiyo hoja ni yeye mwenyewe. Golugwa: Kwa mujibu wa vifungu vya kisheria sifahamu. Katuga: Waambie majaji kama hiyo taarifa ya ushenzi umeileta hapa mahakamani. Golugwa: Sijaileta. Katuga: Mbali ya kuwa katibu wa kanda ya kaskazini waambie majaji kama ukikuwa na wajibu wwa kupokea taarifa kwa makatibu wengine. Golugwa: Nilikuwa ninaratibu na kupokea taarifa kwa makatibu wengine. Katuga: Je, ulieleza mahakama kupokea taarifa zao? Golugwa: Hapana sikueleza Katuga: Waambie majaji wakati ukiwa katibu wa kanda ya kaskazini kama ulikuwa mjumbe wa kamati kuu. Golugwa: Sikuwa mjumbe. Katuga: Waambie majaji aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Bwana Mbwowe alitoa tamko akisema hatutakwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote bila mabadiliko haya ndio maneno uliyonukuuu? Golugwa: Ni kweli Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mwenyekiti alionesha kutoridhishwa na mifumo? Goligwa: Ni kweli. Katuga: Kuna kitu kingine umekisema ukimnukuu mwenyekiti Mbowe Golugwa: Kipi sasa? Katuga: Ninasema kuna lingine alisema mbowe zaidi ya haya? Golugwa: Hapana. Katuga: Hivyo kwa kauli hizi, Mwenyekiti Mbowe aliazimia kwa Chadema kutoshiriki uchaguzi na ilikuwa azimio la kamati kuu. Golugwa: Ni kweli. Katuga: Kuna sehemu yoyote mwenyekiti alitangaza tofauti na kushiriki uchaguzi tunaenda kuuzuia usifanyike? Golugwa: Hayapo. Katuga: Waambie majaji kama kuna maneno ya kwenda kuuvuruga uchaguzi yapo hayapo? Golugwa: Hayapo Katuga: Waambie majaji kama Mbowe alisema tunakwenda kukinukisha vibaya sana. Golugwa: Hayapo. Katuga: Kwakuwa umekuwa mwema. Golugwa: Mimi siwezi kuwa mwema kwako mtu mwenye roho mbaya kama wewe. Katuga: Sasa jitu lenye roho mbaya linakuuliza hivi? Golugwa: Mtu mwema anakujibu. Katuga: je, unajua ni haki kutoshiriki uchaguzi mkuu? Gilugwa: Hapana. Katuga: Waambie majaji unajua ni haki ya kikatiba kushiriki uchaguzi. Golugwa: Ni haki. Katuga: Waambie majaji kwa majibu hayo nakiri nitakuwa sahihi nikisema sio haki kumlazimisha asiyetaka kushiriki uchaguzi kushiriki uchaguzi. Golugwa: Sio haki kumlazimisha. Katuga: Umeelewa kwa mujibubwa katiba gani? Golugwa: Katiba ya Jamuhuri ya Muungano. Shahidi anaendelea kujibu maswali ya upande wa serikali Katuga: Ulisema wewe ni mhasibu Golugwa:Nimefanya kazi za kihasibu Katuga: Wewe sio mhasibu ila ni mtu uliyefanya kazi za kihasibu Golugwa: Sahihi Katuga umesema umekuwa mhasibu tangu mwaka 2001 au umekuwa ukifanya kazi za kihasibu tangu 2001 mahakama ichukue lipi? Golugwa: Nimekuwa nikifanya kazi za kihasibu tangu 2001. Katuga: Kama nimekusikia wewe ndiye mwandishi wa kumbukumbu za vikao vya chama. Golugwa: Ndio. Katuga; Nitakuwa sahihi nikisema wewe ndiye ulichukuwa na minutes za kikao cha tarehe tatu aprili 2025 Golugwa kile kikao hakikuwa na kuchukua minutes. Katuga: Kwa mujibu wa katiba ya Chadema kuna aina ngapi za vikao? Golugwa: Kuna aina mbili za vikao Katuga: Tuambie ni vikao vipi? Golugwa: Vikao vya uchaguzi na utendaji Katuga: Ikitokea mtu akasema aina mbili za vikao Chadema ni vya ndani na hadhara nani anasema ukweli Golugwa: Wote tuko sawa. Katuga: Iambie mahakama vikao vya uchaguzi vinafanana vipi na vikao vya ndani na hadhara.Unaposema vikao vya uchaguzi ulimaanisha nini? Golugwa: Nilizungumzia vikao vya uchaguzi wa chama. Katuga: Sasa vikao vinatofautianaje? Golugwa: Havitofautiani sana. Katuga: je, vinafana havifanani? Golugwa: Havifanani Katuga: Kama nimekusikia umesema hukumbuki masuala ya vikao yako sura ya ngapi? Golugwa: Sikumbuki Katuga; Nikikuambia viko ibara ya sita utakubaliana na mimi? Golugwa: Nikipewa katiba nitasema Katuga: Wasomee majaji ibara ya sita ibara ya ndogo ya pili Golugwa: Kutakuwa na vikao vya aina nne Katuga: Na wewe umewaambia majaji kutakuwa na vikao vya aina mbili sasa majibu yenu na katiba nani anasema ukweli? Golugwa: Hapana Katuga: kwa hiyo nitakuwa sahihi nikisema hujui katiba ya chama chako Golugwa sio kweli. Golugwa: Mawakili wanawapa watu kesi za uongo Katuga: Waambie majaji kama unajua kuulizwa maswali ya dodoso sio suala roho mbaya bali wajibu wa kisheria Golugwa: Nafahamu ila kuna mawakili wana roho mbaya wanawapa watu kesi za uongo Katuga: Unafahamu kesi jinai ni ushahidi na sio ushabiki? Golugwa: Ndio ninafahamu. Katuga: Waambie majaji kama ulisema kuna taarifa zako ziko kwemye public domain. Golugwa: Nilisema habari ya mawakala ndio ipo kwenye public domain. Katuga: Kweli kwamba umekuwa ukizungumza na waandishi wa habari mara kadhaa na ziko kwenye public donain? Golugwa: Ni kweli Katuga: Ni kweli kwamba wewe ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema na ni kutokea lini? Golugwa: Ni kweli kuanzia Januari 2025. Katuga: Ukiwa mjumbe wa kamati kuu ya chadema mwezi wa nane 2026 kamati kuu ilikaa na kujadili mambo mbalimbali? Golugwa: Ni kweli kamati kuu iliketi na kujadili mambo mbalimbali Katuga: Waambie majaji kama ni wewe ulitangaza maazimio ya kamati kuu na iko kwenye public domain. Golugwa: Ni kweli Katuga: Waambie majaji moja ya vitu ulivyo vitangaza ni pamoja na kesi hii Golugwa: Ni kweli Katuga: Katika kuizungumzia kesi hii ulisema mmekusudia mtamtetea mheshimiwa kwa nguvu zote? Golugwa: Sio kweli nilitumia maneno haya viongozi walielekeza muda wao na nguvu katika kumtetea mwenyekiti. Katuga: Tofauti ya kuelekeza nguvu na kutetea kwa nguvu kuna tofauti gani? Golugwa: Maana yake ni kuweka rasilimali zote kwenye jambo moja. Katiga: Nitakuwa sahihi nikisema na wewe ni mmoja wa viongozi hao na umeelekeza nguvu Golugwa: Ndio nimeelekeza nguvu hapa. Katuga: Tofauti ya kiongozi anayeteuliwa na anayechaguliwa. Golugwa: Anayeteuliwa anachaguliwa katikati ya wengi na kuchaguliwa unachaguliwa na wengi Katuga: Naibu katibu mkuu Chadema anapatikanaje? Golugwa: Anateuliwa. Katuga: Anateuliwa na nani? Golugwa: Na mwenyekiti wa chama? Katuga: Ni mwenyekiti gani wa chama aliyekuteua? Golugwa: Na Mh Tundu Lissu Katuga: Katibu mkuu wa chama anapatikanaje Golugwa: Anateuliwa. Katuga: Katibu mkuu wa chama kwa sasa ni nani? Golugwa: Anaitwa John Mnyika Katuga: Ameteuliwa na nani? Golugwa ameteuliwa na mwenyekiti Tundu Lissu Katuga: Hii ni kwa mujibu wa nini? Golugwa: Katiba ya chama. Katuga: Ikitokea mtu akasema yeye uteuzi wake ni wa kamati kuu na sio mwenyekiti atakuwa sahihi? Golugwa: Itakuwa sio sahihi. Siamini ripoti ya Jaji Chande - Shahidi aiambia mahakama Ignas: Kwenye zile kanuni za uchaguzi kuna sehemu ulikutana na neno mkwe wa rais Golugwa: Hakuna Ignas: Umeileza mahakama umewahi kukamatwa na hujawahi kufunguliwa hati ya mashitaka mahakamani Golugwa: Ni kweli Ignas: Ni kweli baada ya kusikilizwa polisi walikuachia Golugwa baada ya mimi kutoa maelezo Ignas: Na mara ya pili unasema ulikamatwa tarehe nane mwezi wa kumi na moja napo uliachiwa baada ya kusikilizwa maelezo yako Golugwa: Ni kweli Ignas: Umeleza elimu yoyote uliyonayo juu ya sheria Golugwa: Sina elimu yoyote ya sheria Ignas: Sasa umepata wapi ujasiri wa kuieleza mahakama mambo ya kisheria Golugwa: Hata Layman anaweza kuongea na yuko mbele yako Ignas: Ulieleza kuhusu ripoti za waangalizi ni za mwaka gani Golugwa: zote ni za mwaka jana Ignas: Wewe ni custodian wa hizo ripoti Golugwa: Nilitafuta na kuzihifadhi Ignas: Umezileta hapa mahakani Golugwa: Hapana Ignas: Hizo ripoti zipo kwa lugha gani Golugwa: kwa kiingereza Ignas: Utakubaliana na mimi wewe sio muandishi wa hizo ripoti Golugwa: Ndio mimi sio muandishi wa hizo ripoti Ignas: Hao walitoa ripoti kuna siku walikuita uzifasiri toka kingereza kwenda kiswahili Golugwa: Kwanini na kwa sababu gani ni tafsiri Ignas: Wewe hapa mahakamani umezielezea kwa kiswahili Golugwa: Ndio Ignas: Utakubaliana na mimi wewe form four ulipata grade gani kingereza Golugwa: Sikumbuki Ignas: Unatatizo la kumbukumbu Golugwa: Ikihitajika ku refresh memory Ignas: Je unafahamu mtu akifasiri inaweza kuharibu maana ya ripoti Golugwa: Kama mtu akitafsiri vibaya yanaweza kuathiriwa au yasiathiriwe Ignas: Umeelaza juu ya uwezo wako kwenye lugha ya kiingereza Golugwa: Sio lazima Ignas: Unafasiri document za kiingereza Golugwa: Kingereza ulipata nini Golugwa C au D Ignas: Sasa na D yako unataka kutafsiri ripoti kubwa kama hizi? Golugwa: Ina shida gani Ignas: Haya tuambie title ya ripoti ya Thabo mbeki kwa kiIngereza ilisemaje Golugwa: Kwa kweli sikumbuki Ignas: Tuje ile ripoti ya SADC wewe mfasiri inaitwaje Golugwa: Kwa kingereza sikumbuki ila inazungumzia Iganas: Kwa kingereza bwana wewe si mkalimani Golugwa: Sikumbuki Ignas: Uliweza kufuatiliwa ripoti ya waangalizi wa Jumuiya ya Afrika mashariki Golugwa: Hapana Ignas: Tukirudi kwenye hii ripoti ya Jaji Chande uliizungumzia jana swali langu ni kwamba una imani na ripoti hii Golugwa: Sina imani nayo Ignas: Kwa hiyo hata kile ulicho kieleza jana huna imani nacho licha kuwa kwenye ripoti ya Jaji Chande Golugwa: Sikubaliana na wewe nilichokueleza mimi nina imani nacho licha kwamba sina imani na ripoti yote Ignas: Inamaana kuna ambavyo vilikupendeza wewe Golugwa: Hapana kitu gani hicho kuzungumzia Ignas: Hebu turudi kwenye kikao cha watia nia uliongea habari ya unyunyu na makapi kulikuwa na habari ya manukato kwemye kikao chenu cha watia nia Golugwa: Anapaswa kupelekea pale anapogombea na kwenye kamati ya rufaa Ignas: Mlishinda mangapi Golugwa: Yalitupiwa mbali sababu ya ushenzi niliosema Ignas: Mliwasilisha hayo malalamiko yenu mahakamani Golugwa: Tuna tambua ila hatukuona haja ya kwenda mahakamani Ignas: Inamaana mlirudhika na maamuzi ya kamati za rufa: Golugwa: Hapana mambo ya kisiasa tunamaliza kisiasa Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu 04.09.2026. Leo tunaendelea na maswali ya dodoso kwa shahidi namba tatu Aman Sam Golugwa ambaye jana alimaliza kutoa ushahidi wake sasa ni zamu ya Jamuhuri kumuhliza maswali.

How it works

Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.

Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.