science_health581 wordsRead on Arc Codex

Kilichonileta hapa sio uhaini ni vita vya kisiasa

Majaji: Mashahidi wengine wanatakiwa kutoka nje hadi pale watakapoitwa. Wangekuwa washtakiwa wangebaki. Jaji Ndunguru: tuambie majina yako kamili Lissu: Naitwa Tundu Antiphas Lissu Lissu: Umri wangu ni miaka 59 Wakili wa mahakama kuu : Kiongozi wa kisiasa na mwenyekiti wa chama cha dini yako ni gani? Lissu: Dini yangu ni Mkatoliki wa Roman na nina apa mbele ya Mahakama hii kuwa ushahidi utakuwa wa ukweli, ukweli mtupu eh Mungu nisaidie. Lissu: Sehemu ya kwanza ya ushahidi wangu ni masuala yanayonihusu mimi mwenyewe kwasababu kosa ninalo shtakiwa nalo ni kubwa. Majaji kama ambavyo nimesema mimi ni kiongozi wa chama kilichoandikiswa rasmi kwa mujibu wa sheria za nchi hii. Nafasi yangu ya sasa ilikuwepo wakati matukio haya yanaendelea mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA. Lissu: Nimekuwa mwenyekiti wa CHADEMA tangu 22 Januari 2025. Nimekaa kwenye nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chama kwa takriban wiki tano au sita ndipo nikakamatwa na kushtakiwa kwa kosa hili. Kwasasa nitasema Hilo maana yake ni nini. Kabla ya hapo nilishikilia nafasi yangu Makamu kwa upande wa Tanzania bara kwa miaka 5 tangu Disemba 2019 hadi Januari tarehe 22 2025 nilipochaguliwa kuwa mwenyekiti. Na kabla ya hapo nilikuwa mwanasheria mkuu wa CHADEMA na mjumbe wa kamati kuu yake ya chama kati ya mwaka 2010 hadi 2017. Lissu: Kwa uhakika ni tarehe 7 Septemba 2017. Hii tarehe ni muhimu kwa hapo baadaye. Kabla ya hapo nilikuwa mkurugezi wa Tiba na haki za binadamu wa CHADEMA tangu Julai 2004 nilipojiunga na chama hadi around Novemba 2011. Na nafasi hiyo ilinifanya kuwa aliyekuwa mwanachama wa kamati wamjumbe wasiokuwa na kura. Kwa ushahidi huu mimi nimekuwa katika uongozi wa CHADEMA katika Ngozi za juu kabisa takriban miaka 20. Lissu anaendelea kujiieleza mbele ya mahakama. Lissu: Nje ya uongozi wa chama niliousema vilevile nimeshikilia nafasi zingine za uongozi kama ifuatavyo: mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu nilichaguliwa kuwa Mbunge katika bunge la jamhuri ya muunguano nikiwakilisha jumbo la singida mashariki Maarufu kama kumbi mashariki. Na nilichaguliwa kwa tiketi ya chadema. Nilichaguliwa kwenye nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 nilitumikia nafasi hiyo Juni 2019. Lissu: Ilikuwaje hadi nikaishia hapa? Narudi kwenye tarehe 7 Septemba 2017, nikiwa Dodoma kwenye vikao vya bunge nilifuatwa kutoka bungeni mpaka kwenye makaazi yangu rasmi na kushamhuliwa na risasi, risasi nyingi sana na watu ambao serikali ya Tanzania inawaita watu wasiojulikana. Lissu: Majaji, kufuatiwa shambulio nilikimbizwa hospitali ya Dodoma na siku hii hiyo kupelekewa nairobi Kenya ambapo nilikaa hospital hadi 6 January 2018. Baada ya hapo nilipelekwa ubelgiji kwaajili ya matibabu zaidi katika hospitali ya Chuo kikuu ya Leuven. Nilitibiwa katika hospitali hiyo hadi Januari 2022. Lissu: Tarehe 29 June 2019 aliyekuwa spika wa bunge ndugai marehemu alitangaza kunifuta ubunge kwasababu nilikuwa mtoro na sijaonekana takriban miaka miwili bungeni hiyo ndiyo sababu iliyopelekea nisimalize muhula wangu wa pili kama mbunge. Lissu: Na niongeze tu kuwa katika kesi hii licha ya kuwa mbunge nakuumizwa vibaya nikiwa kazini bunge na serikali ya Tanzania ilikataaa katakata kulipa gharama ya matibabu yangu. Sikupewa hata senti moja. Lissu: Vilevile nilikuwa Msemaji mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa masuala ya katiba na sheria, muungano, pamoja na mwanasheria mkuu mwandamizi wa Mwanasheria Mkuu. Lissu: Majaji ningependa Mahakama irekodi kuwa nilifanya kazi yangu ya ubunge kwa heshima kubwa na umahiri. Majaji nilikuwa kipindi hicho hicho cha 2011-2015 nilikuwa mjumbe wa bunge maalum na katiba. Na kwa kipindi hicho bungeni niliongoza harakati za kupigania katiba mpya na mfumo huru wa uchaguzi. Kilicho nileta hapa sio uhaini ni mgogoro wa katiba mpya, ni vita vya kisiasa.

How it works

Once you click Generate, Ollama reads this article and crafts 5 comprehension questions. Your answers are graded against the article content — general knowledge won't be enough. Score 70+ to count toward your certificate.

Questions are cached — you'll always get the same 5 for this article.